Tuwe wawazi tulijenge taifa uwazi na ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe wawazi tulijenge taifa uwazi na ukweli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anyisile Obheli, Jan 22, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Asalam aley khum ndugu Watanzania, ni siku ya kwanza ya mwaka 2010
  hii inatuonesha kuwa tayari tumeumaliza mwaka wa 48 tangu nchi yetu ipate uhuru,
  tuanaingia mwaka wa 49. Pamoja na hayo taifa la Tanzania limepitia vipindi
  mbali mbali vya wananchi wake kutawali na kundi moja la chama kimoja
  cha CCM tangu kuwaondoa watawala wa Kizungu ambao japo waliiendesha
  nchi kwa faida yao lakini pia Watawaliwa walikuwa na afadhali ya ukame mahitaji,
  ndiyo kilikuwa ni kipindi mtu anajaliwa kwa utu wake ukilinganisha na kipindi
  walipoondolewa na nchi kumilikiwa na kundi walijiita wana wa CCM ambao
  hawa waliingia katika uongozi kwa maslahi yao zaidi na maslahi ya chama
  chao cha CCM na si kwa ajili ya taifa na wananchi kwa ujumla.
  Utawala wa Ulikuwa ukiongozwa na Mtu aliyejiita Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE
  chini ya serikali ya CCM Utawala ambao haukuwapenda sana wazalendo hata kufika hatua
  ya kutaifisha mali zao kwa kuwabambikia majina ya wahujumu uchumi, na wale
  walionekana kuwa wasomi zaidi ama kulipenda sana taifa lao basi walifikia hatua ya
  'kutaifishwa' uhai wao ama Kulazimishwa kuishi chini kukubari kila jambo yaani
  'ndiyo mzee ama tawile'Kutokana na tabia ya CCM kutopenda usawa kwa kudumisha utu,
  basi mtu yeyote aliyeonekana kupinga alilazimishwa kufa kwa ridhaa yake au kuuliwa,
  nasema kuuliwa kwa sababu ikiwa mtu amesema ukweli hupoteza uhai katika Mazingira
  ambayo mtu yeyote mwenye uchungu na taifa hawezi kuridhishwa nayo, ambapo hata
  serikali hainekani kustuka ama kutaka kufanya uchunguzi wa nini kimefanyika.
  Siogopi kusema haya kwa sababu demoklasia yangu inaniruhusu kusema ingawaje
  mara nyingi ukweli huwafanya watu wafe ama wauliwe.
  HATA BWANA YESU alikufa kwa sababu ya kuibeba kweli na kuileta duniani
  wale waliopenda uovu walipanga njama za kumwua wakisaidiana uongozi
  wa serikali ya Kiroma chini ya mtu aliyejiita Pilato.Lipi lililo jepesi ukiifia kweli
  ama uishi kwa kuutukunza uuaji, ushenzi,ukandamizaji, udharirishaji na utawala wa kimabavu?
  Ama kuna kuwatunza viongozi vipofu na kuwafanya watoto wao wanywe Chai ya maziwa na boflo,
  harafu wa kwetu wanywe chai kavu na yenyewe kwa bahati mbaya? Hili haliwezeka kwangu
  mimi ni heri kuiifia kweli ile ninayoijua,Hebu twende taratibu tukianza na Mazingira
  ya kifo cha mzee wetu Edward Moringe Sokoine, kuna mtu mwingine Mzee Korimba,
  kuna Imran Kombe, kuna akina Kigoma Ali Malima, si hao tu nani anajua mazingira
  ya kifo cha mzee Omar Alli Juma ni vifo vyenye mazingira ya utata, lakini serikali ya
  Chama cha Mapinduzi imenyaza kimya haitwambii chochote si wengine hatujui
  hapana we know every thing evil done by CCM katika kulinda na kutetea ushenzi
  na udikiteta wake madarakani.
  Ni nani anajua Abeid Amani Karume alipigwa risasi na kundi la vita gani na kutoka
  wapi tangu Nyerere hata sasa bado kuna uozo mkubwa unaofanywa na CCM kwa
  watanzania wanyonge ambao wameishia kuburuzwa hovyo na washenzi wachache
  tu kwa maslahi ya vizazi vyao. Hivi leo tuiambie serikali ya Tanzania chini ya chama
  cha mapinduzi ituandalie ripoti ya matukio mbali mbali itatuambie hivi karibuni
  tumeshuhudia mabomu yakilipuliwa kwa makusudi Mbagala hakuna hata la kuuridhisha
  umma kwa maelezo Umefika wakati wa kuambiana ukweli bila hata ya kuogopana wala
  kuoneana aibu kama kuuana heri, kuangalia ndugu jamaa zetu wakipoteza maisha kwa
  ujinga tu, haiwezekani, viongozi na watanzania wengi wanaujua ukweli hawataki kuweka
  kwa kuogopa kufishwa, nani kakwambia mtu ataishi miaka yoote hapa duniani?
  Maana ni heri yule aogopaye kumkosea Mwenyezi Mungu kuliko kumwogopa
  mwanadamu tu, kwani mwanadamu ni nani mbele za Mungu nasema tena na
  tena kama kufa tutakufa woote lakini kweli lazima tuitenge na giza kwa msaada
  wa Mungu, haiwezekani kabisa lazima maana imeandikwa 'msiwaogope
  hao wawezao kuua mwili wasiweze kuiua na roho, bali mwogopeni yule
  awezaye kuua mwili na roho pia' yaani Mungu tu.
  Na lile lililofanywa gizani litawekwa peupe. Na vibaraka wengi wa CCM ni
  waota ndoto za mizimu, usishangae ajitokeza mtu muaguzi na utabili wake
  wa kipepo na kuwakatisha tamaa wengine kwa kuandaa mazingira ya wazi wazi
  ya kuua mtu muhimu atakaye tokea kuipinga CCM katika uchaguzi ujao, hizo ni
  tantata lila za uongo tu, na uzushi tu ili baadae wakiua mtu tuanze kusema aaa!
  alitabiri Shekh Yahya, bila aibu vingozi wenye mikataba na CCM ya muda mrefu
  wanaanza kuwashauri watanzania kuto wapuza wasoma nyota na wafuasi wa mapepo
  na mashetani ya uuaji,Safari hii ni zamu yake Hakuna kiongozi yeyote wala Mgombea
  yeyote atakaye jitokeza kuipinga CCM akafariki, Sasa ni wakati wa kufa mwenyewe
  Shekh Yahya na kundi lake la uuwaji.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA BARIKI WATU WAKE
   
Loading...