Tuwe wakweli, hivi mkeo au mmeo ana mapungufu yapi?

Nathan Jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,437
1,875
Halo asubuhi ikoje huko,?

Naelekea kwenye mada moja kwa moja,

Najua hakuna binadamu aliyekamilika,
Kila mtu ana mapungufu yAke

Mwenzangu ana mapungufu haya
1. Mkikorofishana ananuna siku nzima hata kwa kitu kidogo zaweza pita hata siku tatu,

2. Tukikorofishana ukimbilia kuniblock whatsap na kuniweka blacklist kwenye calls za kawaida ,nami nikikausha anakuja mwenyewe baada ya siku kama tatu, atapiga eti "nimeona missed call yako unasemaje haha dah"

Au atatuma empty Sms kusikilizia kama ntauliza,


3. Hataki niwape marafiki zangu hela yaan hataki mpaka nijifiche au niwape kwa kuficha,


Je wa kwako ana mapungufu yapi?
 
Mi wa kwangu wa sasa afadhali ,ila anakibri,

Waliopita alikuwa anapenda hela kupitiliza hata nkimfanyia jambo hariziki,

Mwingine tukigombana anakimbilia kuwaweka status mbwana zake wa zamani,
 
Kuwashauri jinsi ya kuyatatua
Sasa umeshakiri kua "hakuna binadamu aliyekamilika, kila mtu ana mapungufu yaje" halafu unasema utashauri jinsi ya kuyatatua!

Na hapo hapo wewe umetaja mapungufu ya mkeo?! Si ungeanza kuyatatua yako kwanza? Unazima kwa jirani wakati kwako kunaungua?

Kila binadamu ana mapungufu yake,tunatakiwa kuvumiliana tu na kusameheana.
 
Back
Top Bottom