Tuwe makini na wasichana wa kazi (House girls)

KICHINJIO 15

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
823
628
Habari za Weekend, Wadau!

Kuna baadhi ya wasichana wa kazi huonekana wapole, watiifu, wachapa kazi, n.k kiasi ambacho mabosi wao huamua kuwaongezea mishahara au kuwapa zawadi yoyote ile to show their appreciation kwa hao wadada.

Kwa bahati mbaya sana baadhi ya wafanyakazi hao ni wachawi na mabosi huwa hawajui hadi pale jambo baya linapokuja tokea kwenye familia zao kutokana na uchawi wa wafanyakazi hao.

Najua wengine humu walishawahi kuishi na wadada wa namna hiyo na zahma zikawakumba.

Nilisimuliwa mkasa mmoja na jamaa yangu kuhusiana na wadada hawa:

Familia moja ilikuwa na msichana wa kazi aliyependwa na kuaminiwa sana na kila mwanafamilia kwa sababu Kila kitu kilifanywa kwa usahihi na kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, yule binti alikuwa ana uwezo wa kupendekeza kitu kwa bosi wake na akasikilizwa. Hivyo, kila mama mwenye nyumba alipotaka kuwanunulia nguo watoto wake (wadogo wawili ke na me) HG alipendekeza wanunuliwe nguo nyekundu. Alikubaliwa.

Hata usiku alikuwa akilala nao na walikuwa wakimpenda sana.
Baadaye familia ikawa inaandamwa na mikosi na maradhi mfululizo kiasi cha kuitia familia umaskini.

Wale watu wakamwita mtumishi wa Mungu, akawaombea wanafamilia wote na ndipo walipogundua kuwa yule HG ni mchawi na ndo chanzo kikubwa cha matatizo hayo (maana alikiri mwenyew baada ya kuungua na moto wa Roho Mtakatifu.)
Akasema na mengine mengi tu.
1. Kazi zote mle ndani huwa hafanyi. Huwafanyisha mabosi wake.
2.Watoto alishaanza kuwafundisha uchawi na ndo kisa cha kuwachagulia nguo nyekundu.
3. Ameshawahi kuwalisha nyama za binadamu wao wakijua wanakula nyama ya ngómbe au noah.
4. Uchawi huo alijifunza kwa bibi yake (mzaa mama)

Hivyo, ili tuwe salama ni muhimu kufanya yafuatayo:
1. Tujaribu kujua familia zilizowalea na kuwakuza kabla ya kuwaajiri.
2. Tuwachunguze kwa makini tunapokuwa nao.
3. Kubwa zaidi tumwombe Mungu kabla ya kuwaajiri na hata tunapoishi nao ili tuyaone matendo yao ya giza kwa jicho la rohoni.

Angalizo: Usianze kumhisi vibaya msichana wako wa kazi
 
Nimeishi nao watatu wenye tabia hizo na mmoja tu nilimfukuza alipoanza kunifanyia vitimbi hadhani , siku ya kwanza alikosa Mimi nikawa namsema huku nimeshika kabati la vyombo nimeshika nataka kufungua kioo kikapasuka nikageuka haraka kumuangalia nikamuona anatingisha kichwa kama anaitikia siwezi kuhadithia nilichokiona kwake nikamwambia weeee nitakufukuza kazi hakujibu akaondoka, siku ya pili nimetoka kazini naingia tu akaniita yupo jikoni ananiambia "we mama muondoe mwanao haraka kabla sijamuua" yaani hiyo ndio salamu duuu nilisikia matumbo yanakata (akina mama wananielewa namaanisha nini) nikahisi naishiwa nguvu ila nikamuuliza kwa sauti ya upole kwa nini umuue akajibu simpendi na nikiosha vyombo anachafua, nikamwambia sawa nitamuhamisha aliporudi mtoto nikampa pesa akaenda nunua chips akala nikalala naye chumbani Saa kumi na mbili asubuhi nimeshavaa nikamwamsha nikamwambia simama beba vitu vyako nikuridishe nilipokutoa akasema siendi, nikamwambia toka mwanangu abaki siwezi kumtoa yeye utaka wewe? Nikamrudisha nilipomtoa
 
Nimeishi nao watatu kwenye tabia hizo na mmoja tu nilimfukuza alipoanza kumufanyia vitimbi hadhani , siku ya kwanza alikosa Mimi nakawa namsema huko nimeshika kabati la vyombo nimeshika unataka kufungua kioo kikapasuka nikageuka haraka kumuangalia nikamuona anatingisha kichwa kama anaitikia siwezi kuhadithia nilichokiona kwake nikamwambia were nitakufukuza kazi hakujibu akaondoka, siku ya pili nimetoka kazini naingia tu akaniita yupo jikoni ananiambia "mama muondoe mwanao haraka kabla sijamuua" yaani hiyo ndio salamu duuu nilisikia matumbo yanakata (akina mama wananielewa namaanisha nini) nikahisi naishiwa nguvu bila nikamuuliza kwa sauti ya upole kwa nini umuue akajibu simpendi na nikiosha vyombo anachafua, nikamwambia sawa nitamuhamisha aliporudi mtoto nikampa pesa akaenda nunua chips akala nikalala naye chumbani Saa kumi asubuhi nimeshavaa nikamwamsha nikamwambia simama beba vitu vyako nikuridishe nilipokutoa akasema siendi, nikamwambia toka mwanangu abaki siwezi kumtoa yeye utaka wewe? Nikamrudisha nilipomtoa
Pole mkuu.
Kuna mmoja aliuliwa mwanae, kimazingara. Baada ya wk moja yule mama alichokikuta home nusura azimie. Alikwenda kazini asbh halafu akarudu ghafla home kuchukua kitu fulani alichokisahau. Akamkuta mdada uwanjani anafagia.
Akamsalimia na kuingia ndani. Nako akamkuta mdada akifanya usafi. Kwa mshangao akaingia jikoni, nako akamkuta mdada huyo huyo akiosha vyombo.
Kumbe yule dada alijiweka ktk nafsi 3 kichawi.
 
Hizi imani zenu za kushirikina...
Hata Mimi nilikuwa siamini ndio maana hao wengine sikuwafukuza waliondoka wenyewe na huyu wa tatu nilimtoa baada ya kunitamkia atamuua mwanangu, pia hata kama huna imani ipo siku atatoa ishara utajua tu, kikubwa hapo mtoa mada katoa ushauri nzuri sana anayetaka aufuate asiyeamini aokote hivyo vidada aweke ndani
 
We waache wasio amini yakija wakuta watalia kikwao.
 
Pole mkuu.
Kuna mmoja aliuliwa mwanae, kimazingara. Baada ya wk moja yule mama alichokikuta home nusura azimie. Alikwenda kazini asbh halafu akarudu ghafla home kuchukua kitu fulani alichokisahau. Akamkuta mdada uwanjani anafagia.
Akamsalimia na kuingia ndani. Nako akamkuta mdada akifanya usafi. Kwa mshangao akaingia jikoni, nako akamkuta mdada huyo huyo akiosha vyombo.
Kumbe yule dada alijiweka ktk nafsi 3 kichawi.
Nimemtumiwa hiyo jana binti anakiri mwenyewe
 
Nimeishi nao watatu wenye tabia hizo na mmoja tu nilimfukuza alipoanza kunifanyia vitimbi hadhani , siku ya kwanza alikosa Mimi nikawa namsema huku nimeshika kabati la vyombo nimeshika nataka kufungua kioo kikapasuka nikageuka haraka kumuangalia nikamuona anatingisha kichwa kama anaitikia siwezi kuhadithia nilichokiona kwake nikamwambia weeee nitakufukuza kazi hakujibu akaondoka, siku ya pili nimetoka kazini naingia tu akaniita yupo jikoni ananiambia "we mama muondoe mwanao haraka kabla sijamuua" yaani hiyo ndio salamu duuu nilisikia matumbo yanakata (akina mama wananielewa namaanisha nini) nikahisi naishiwa nguvu ila nikamuuliza kwa sauti ya upole kwa nini umuue akajibu simpendi na nikiosha vyombo anachafua, nikamwambia sawa nitamuhamisha aliporudi mtoto nikampa pesa akaenda nunua chips akala nikalala naye chumbani Saa kumi na mbili asubuhi nimeshavaa nikamwamsha nikamwambia simama beba vitu vyako nikuridishe nilipokutoa akasema siendi, nikamwambia toka mwanangu abaki siwezi kumtoa yeye utaka wewe? Nikamrudisha nilipomtoa
Jumatatu mpaka Jumatano nilisikiliza kisa cha House girl Mchawi E-FM, Niliuzunika Sana kwa jinsi alivyomuua kichawi mtoto WA Boss wake! Ningekua mm ndo Baba WA mtoto, muda huu niko jela kwa kesi ya Mauaji!
 
Pole mkuu.
Kuna mmoja aliuliwa mwanae, kimazingara. Baada ya wk moja yule mama alichokikuta home nusura azimie. Alikwenda kazini asbh halafu akarudu ghafla home kuchukua kitu fulani alichokisahau. Akamkuta mdada uwanjani anafagia.
Akamsalimia na kuingia ndani. Nako akamkuta mdada akifanya usafi. Kwa mshangao akaingia jikoni, nako akamkuta mdada huyo huyo akiosha vyombo.
Kumbe yule dada alijiweka ktk nafsi 3 kichawi.
Nilisikiliza hicho kipindi E-FM, Wachawi hawatakiwi kuishi, japo binti ilibidi awe mchawi kumuokoa Baba yake....... Na sasa anasema kaokoka! Dah
 
Back
Top Bottom