MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,238
- 50,413
Nimefurahi sana kuona hatua ambayo tumefikia kama nchi kwenye masuala ya SGR. Treni zetu japo zitawekwa umeme hapo baadaye, lakini kwa sasa zitakua zinachana mbuga kwa kasi ya 120km/h
Sasa hapo ndio wasiwasi wangu uliopo, maana Waafrika sidhani kama tupo tayari na mambo haya ya kasi. Juzi nimeona taarifa za Tanzania treni na behewa za abiria zimebinuka, bahati hazikua kwenye mwendo kasi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.
Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.
“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.
Breaking News!! TRENI YA MWENDO WA HARAKA - DELUX YAANGUKA PWANI IKITOKA KIGOMA KWENDA DAR ..TAZAMA PICHA | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today