Tuwe makini kabla malaika hajazima mtandao

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,257
21,286
Shaka sina sote tunakumbuka ile kauli ya kushukiwa na Malaika Mzima Mitandao, Maandiko matakatifu yanafunua kwamba anachozungumza mtu ndicho kimejaa nafsini mwake.

Lile tamko lilizungumzwa kama utani lakini ndani yake ikiwa ulimtazama kwa makini hakukuwa na chembe ya utani hata tone, lisemwalo lipo, kama halipo linjiani.

Tusitegemee kiuhalisia kua itazimwa kweli VUUUUUP.. Ila inaweza kua ni lugha ya picha kuashiria ufinyu wa uhuru wa kujimwaya mwaya mtandaoni. Jana inasemekana simu zimeanza kurekodiwa, kesho lolote laweza kutokea.

So huenda Malaika akakuzima wewe au mimi tusipokua makini, automatically unajikuta huna hamu kabisa na haya mambo ya mitandaoni. Lakini pia haimaanishi tuwe wanyonge ila tuwe makini.

Ila sasa, tujitahidi kutumia fursa ya kimtandao iliyopo mbele yetu maana huwezi kujua kesho KIONGOZI KABISA akiamka asubuhi ataamkaje,

Iweni wepesi kusikia kuliko kuongea.
 
"Malaika alikataa ila sasa amekubali'. Juzi alituomba vyombo vya habari pamoja na mitandao tuwe mabalozi wazuri... Kwa kweli hili nililiona kama ushindi...Sasa hivi Malaika anaifurahia mitandao kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele kupongeza juhudi zake na kumsifia kwa kila anachokifanya. Naona ameelewa kuwa mitandao haina anything personal against him....

Kwa hiyo suala la kuzimwa kwa mitandao halipo tena. Hilo kwa sasa lisahau... Malaika mwenyewe keshafanya mitandao kuwa mahali pake pa kudumu pa kupatia Ubuyu....
 
Hamkani si shwari tena. Hivi lile katazo la Waandishi wasionekane maeneo yale mmelielewa?
Oh oops, Nimesahau tena. Niwe mwepesi wa kuona tu.
 
"Malaika alikataa ila sasa amekubali'. Juzi alituomba vyombo vya habari pamoja na mitandao tuwe mabalozi wazuri... Kwa kweli hili nililiona kama ushindi...Sasa hivi Malaika anaifurahia mitandao kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele kupongeza juhudi zake na kumsifia kwa kila anachokifanya. Naona ameelewa kuwa mitandao haina anything personal against him....

Kwa hiyo suala la kuzimwa kwa mitandao halipo tena. Hilo kwa sasa lisahau... Malaika mwenyewe keshafanya mitandao kuwa mahali pake pa kudumu pa kupatia Ubuyu....
Technicaly speaking..
 
Wakizima tusipo nunua vocha na kujiunga vifurushi voda tigo airtel halotel wale wapi na wenye blog's wale wapi au anataka ongezeko la ma jobless mtaani uyo malaika hajatokea mbinguni labda shimoni ata jf so max atakosa ajira aache utani uyo malaika mweusi apo ajue anagusa ugali wa watz
 
Akimbizane na waimba kwaya+waosha magari.
Saa hizi atakuwa Instagram anacheki udaku coz ndiyo shughuli anazozipenda
 
Sijui waafrica tuna nini mtu akipata nafasi lazima amnyanyase mwenzake hata kama hana madhara.Nashangaa badala ya kujenga viwanda kila siku tunatafutana ubaya.Kila siku ni kutafuta laaana tu.
 
Kama wameanza kurekodi simu inabidi kuwa makini sana kwenye mazungumzo, japo nasikitika zoezi la kusajili line za simu liliendeshwa kizembe sana, taarifa za watumiaji wengine ni za uongo, kitu kinachofanya kumtambua mmiliki halisi wa line kuwa na utata.
 
Unajua ukisukumwa sana mwisho ukakuta kuna ukuta,unakuwa hauna namna zaidi ya kugeuka na kupambana.Icho ndicho viongozi wetu wanataka kutulazimisha kufanya.Iko siku,nasema,iko siku yaja ambapo Watz tunao waona wanyonge they will rise na hapo ndipo tutajua kimya kingi kina mshindo mkubwa.
 
Sometimes nawaza ikifika mwisho wa huo ukuta itakuaje, Ila sisi ni wapole sana.
 
Sijui waafrica tuna nini mtu akipata nafasi lazima amnyanyase mwenzake hata kama hana madhara.Nashangaa badala ya kujenga viwanda kila siku tunatafutana ubaya.Kila siku ni kutafuta laaana tu.
Mkuu, wa kujenga viwanda alikua ni nyerere tu.
 
NASHAURI MLETA MADA AACHE KUTUMIA TUMBO KUFIKIRI
Unaniona mjinga sana kwakua unanufaika na mfumo, ila amini amini nakwambia, hakika Kiongozi wetu akiamua lake hatosikia la muadhini, mteka maji wala shekh, hanaga undugu na mtu wa uchama, kumbuka Yusuph Manji ni diwani kwa ticket ya chama chenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom