Tuwe karibu na wanawake na kuwajali nyakati zote

mxsdk

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,585
2,049
Hivi karibuni nilienda hospitali moja hapa Tanga maeneo ya Mjini kati (JINA KAPUNI SITOLITAJA) kumtembelea rafiki yangu aliyekuwa amelazwa. Nilikuwa nimekaa mapokezi nikisubiri ruhusa ya kuingia wodini.

Ndipo niliposikia kelele za kilio cha haja kutoka dirisha la chumba nilichokuwa nikitizama nacho na nilipokaa.

Niliingiwa na woga na nikatoa macho kweli na kutamani kukimbia niahirishe Visit yangu, Kile kilio hakikuwa cha kawaida nikajikuta Nikimuuliza dada wa mapokezi ni nini kinaendelea katika kile chumba?

Yule dada akanijibu, "Hapo ni Labour kuna mwanamke anajifungua." Dah sijawahi sikia au shuhudia mwanamke akiwa anajifungua zaidi ya kuangalia tu kwenye sinema.
Nikafikiri ni kiasi gani kile kilio kinamaanisha maumivu yalivyo makubwa.

Wakati nikiendelea kufikiria, kukawa kimya na mwanaume ambae bila shaka alikuwa ni daktari alikitoka na kubamiza mlango akaja tulipokuwa tumekaa akiwa na sura ya huzuni.

Na baadae nilipata taarifa kwamba yule mwanamke alifariki yeye pamoja na mtoto wake. Chanzo kikubwa ni kwamba mwanamke hakupata kuhudumiwa vema kipindi cha ujauzito.

NIMEANDIKA HAYA KWA NINI?
Hakuna kipindi ambacho mwanamke wako anakuhitaji zaidi kama kipindi hiki cha ujauzito, kujifungua ni kupigania maisha aitha ya mama, mtoto au ya wote.

Kuwa karibu na mkeo ktk kipindi cha ujauzito, uwepo pale anapokuhitaji. Usimpe sononeko la moyo. Mpe faraja na umfurahishe. Wanaume wengi hukoleza sana kuchepuka kipindi wake zao wanapokuwa wajawazito.

Kiteteo chao kikubwa huwa ni kwamba wake zao wamekuwa rafu sana kipindi cha ujauzito bila kutambua kwamba ni kipindi ambacho hata saikolojia ya mwanamke hubadilika kutokana na ujauzito.

Ni kweli tendo la ndoa huwa tunalifurahia ila pia Jaribuni kuwaelewa na kuwa nao karibu wanapokuwa wajawazito. Hii huwapa faraja na hata mtoto tumboni hukua vema.
Zile kelele za maumivu ya yule mwanamke nilizozisikia hospitalini pamoja na taarifa za kifo chake, ziliniongezea jambo kichwani, kwamba kipindi cha ujauzito, ndicho kipindi ambacho ninapohitajika kuwa karibu na mwanamke wangu kuliko kipindi chochote kile.
HAKIKA TUKIO lile lilikuwa somo kubwa sana kwangu.

BUSARA YANGU: "Real men will never walk-out on their pregnant women"
Mungu awasaidie wanawake kwa magumu yote mnayopitia na pia abariki tumbo lenu la uzazi!
AMEN.
 
dcfecc4d00ed50aada08fc0ff6e8759d.jpg
 
Kuna mdada nilikua namtembeza kimazoezi kipindi cha ujauzito (siyo mtu wangu).

Tulikua tunaongea mengi, ishu zingine ambazo sikutakiwa kuzijua nilizijua kipindi hiko.
Naamini Kuna bondi fulani unatengeneza kwa mwanamke kipindi hiki, najisikia vibaya ambaye alitakiwa atengeneze hiyo bondi hakuepo kipindi anahitajika.

Kama mwenzi wako ana mimba yale mazoezi fanya naye tu, hua inakua poa sanaaaaaa.
 
Hivi karibuni nilienda hospitali moja hapa Tanga maeneo ya Mjini kati (JINA KAPUNI SITOLITAJA) kumtembelea rafiki yangu aliyekuwa amelazwa. Nilikuwa nimekaa mapokezi nikisubiri ruhusa ya kuingia wodini.

Ndipo niliposikia kelele za kilio cha haja kutoka dirisha la chumba nilichokuwa nikitizama nacho na nilipokaa.

Niliingiwa na woga na nikatoa macho kweli na kutamani kukimbia niahirishe Visit yangu, Kile kilio hakikuwa cha kawaida nikajikuta Nikimuuliza dada wa mapokezi ni nini kinaendelea katika kile chumba?

Yule dada akanijibu, "Hapo ni Labour kuna mwanamke anajifungua." Dah sijawahi sikia au shuhudia mwanamke akiwa anajifungua zaidi ya kuangalia tu kwenye sinema.
Nikafikiri ni kiasi gani kile kilio kinamaanisha maumivu yalivyo makubwa.

Wakati nikiendelea kufikiria, kukawa kimya na mwanaume ambae bila shaka alikuwa ni daktari alikitoka na kubamiza mlango akaja tulipokuwa tumekaa akiwa na sura ya huzuni.

Na baadae nilipata taarifa kwamba yule mwanamke alifariki yeye pamoja na mtoto wake. Chanzo kikubwa ni kwamba mwanamke hakupata kuhudumiwa vema kipindi cha ujauzito.

NIMEANDIKA HAYA KWA NINI?
Hakuna kipindi ambacho mwanamke wako anakuhitaji zaidi kama kipindi hiki cha ujauzito, kujifungua ni kupigania maisha aitha ya mama, mtoto au ya wote.

Kuwa karibu na mkeo ktk kipindi cha ujauzito, uwepo pale anapokuhitaji. Usimpe sononeko la moyo. Mpe faraja na umfurahishe. Wanaume wengi hukoleza sana kuchepuka kipindi wake zao wanapokuwa wajawazito.

Kiteteo chao kikubwa huwa ni kwamba wake zao wamekuwa rafu sana kipindi cha ujauzito bila kutambua kwamba ni kipindi ambacho hata saikolojia ya mwanamke hubadilika kutokana na ujauzito.

Ni kweli tendo la ndoa huwa tunalifurahia ila pia Jaribuni kuwaelewa na kuwa nao karibu wanapokuwa wajawazito. Hii huwapa faraja na hata mtoto tumboni hukua vema.
Zile kelele za maumivu ya yule mwanamke nilizozisikia hospitalini pamoja na taarifa za kifo chake, ziliniongezea jambo kichwani, kwamba kipindi cha ujauzito, ndicho kipindi ambacho ninapohitajika kuwa karibu na mwanamke wangu kuliko kipindi chochote kile.
HAKIKA TUKIO lile lilikuwa somo kubwa sana kwangu.

BUSARA YANGU: "Real men will never walk-out on their pregnant women"
Mungu awasaidie wanawake kwa magumu yote mnayopitia na pia abariki tumbo lenu la uzazi!
AMEN.
Kweli kabisaa
 
Sipati picha wanaume wakiruhusiwa kuingia chumba cha labour na kujionea kazi inayofanywa reaction yao itakuwaje.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom