Yaani CD ya Iris iuzwe 5000 na CD ya bongo movie iuzwe 5000 yaani niache Iris nichukue bongo movie ni kama vile dagaa wa kigoma wauzwe bei sawa na wa mwanza nani atawanunua wa mwanza?
Mfano season mpya ya prison break iliyotoka leo hii iwekwe sokoni na picha zenu za bongo movie tuone kama haitouzika
Mbona diamond kwenye industry ya muziki na kampuni yake ya wcb anafanya vizuri na mashabiki wake wananunua kazi zake
Diamond anatumia kiasi kikubwa cha pesa kutengeneza quality music hawa bongo vilaza wana act kijinga yaani Ray ni director,editor,author,main character yeye yaani kila kitu yeye khaaa
Wakati movie za nje zikiisha mwishoni utakuta list ndefu ya ya presenters ,waigizaji ,waliohusika nk lakini bongolala utakuta list fupi
Movie za nje huchukua muda mpaka inakuwa inaisha lakini huku kwetu miezi 4 movie imeisha
Mwishoni hata wafanyaje bongo movie itabaki vile vile
Waombe tu housegals waongezeke na wanunue kazi zao kwa wingi wawashawishi
Hebu tizama tamthilia za wafilipino,Venezuela na mexico utafananisha na upuuzi wa bongo movie
Movie za nje ni kama dagaa wa kigoma wawekee price tag ya 5000 na bongo movie dagaa wa mwanza 5000 aah kila mtu atakimbilia dagaa wa kigoma