jilala gabriely
Member
- Jun 8, 2013
- 42
- 35
Wanajamvi katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maandamano na matamko mengi kuhusu kazi za bongo movie na movie za nje (kikorea) lakini watu hawa wanaoandamana walikosa uwakilishwaji mzuri wa hoja zao mpaka kufika mahali watu kutowaelewa.
UKWELI ni kwamba ni kwel kazi za movie za nje zinaua soko la movie za ndani.
Tunafahamu hitaji(demand) la bidhaa katika soko inategemea sana na vitu vifuatavyo'
Bei ya bidhaa yenyewe(price of commodity). Hapa tuwe wawazi kama bidhaa itauzwa kwa bei kubwa sokoni basi hitaji lake litashuka sana (elastic demand). Hii haiwadhuru bongo movie.
Bei ya bidhaa ya mfanano sokoni(price of related goods). Hii ndio inayowaumiza bongo movie
.
Bei ya bidhaa ya mfanano sokoni (movie za nje)ikiwa ndogo kuliko bidhaa yako(bongo movie) basi wanunuzi watapendelea sana kununua ile bidhaa nyingine(movie za nje)kuliko bidhaa yako (filamu za bongo)sokoni. Hata bongo muvi wakitengeneza filamu bora za aina gani haziwezi kulifikia soko la muvi za nje.
Tuungane tuiambie serikali kitu kimoja ifanye filamu za nje nazo zilipe kodi kwa serikali na kupitia hatua zote kama wanazopitia bongo muvi (hapa itafanya bei kupanda na kufanana na bei ya filamu ya bongo) au serikali iwaondolee kodi kabisa bongo movie ili bei za filamu sokoni zifanane ili kuwe na ushindani. Baada ya apo tuwaachie bongo movie waboreshe ubora wa kazi zao.
Maoni yako mdau.