Tuwapongeze Polisi,Ila Watazamwe Upya..

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Nikiwa raia wa kawaida kabisa kwa dhati nina ushauri kwa Viongozi waandamizi ..

Ni ukweli usiopingika idadi ya raia wa Tanzania inakadiriwa kuwa ni karibu Milioni 50 kwa sasa.
Ni kweli kabisa idadi ya polisi hapa nchini haifiki 90000,Polisi wa kawaida,FFU na Askari wa Usalama Barabarani.Kwa haraka makadirio ya wastani wa karibu watu 550 wanalindwa na polisi mmoja.

Ni ukweli usiopingika Polisi wanafanya kazi ngumu kwa masaa yasio na idadi ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao vinatamalaki..Kwa mijini polisi ndio wanaosaidia kuondosha misongamano itokanayo na foleni,misafara ..Bila kusahau ndio wanaolinda mitihani ya kitaifa,michakato ya uchaguzi kisiasa..,Wanakusanya mapato kupitia tozo,adhabu,,,,

Polisi hawana overtime,polisi mishahara yao ni midogo kwa kiwango cha kuwafanya iwe rahisi kwao kushawishiwa kupokea rushwa.Bila kusahau kutokana na changamoto za kibajeti bado makazi yao hayatoshelezi mahitaji halisi hivyo wengi kujikuta wakiishi uraiani ambako hawaonekani kuwa rafiki wa raia..

NINI KIFANYIKE?

  1. Waongezewe marupurupu ili kuwapa hamasa ya kufanya kazi kwa uzalendo ikiwemo overtime,Incentives chanya.
  2. Utaratibu ufanyike ili kupitia Shirika la Bima la Taifa {NIC} wawekewe bima ya maisha hasa kutokana na mazingira hatarishi ya utekelezaji wa baadhi ya majukumu yao ya kila siku {Kupambana na wahalifu,Majambazi,utapeli,wizi,uvamizi n.k}.
  3. Wawezeshwe kwa kupewa vitendea kazi vya kisasa vinavyoweza kuwasaidia kukabiliana na uhalifu wa namna nyingi pasipo kutumia nguvu kubwa,idadi kubwa..bali kisayansi na kiteknologia-Isisubiliwe wakati wa Uchaguzi pekee.
  4. Semina elekezi za kuwajenga kiufahamu,kitaaluma,kiteknolojia ziwepo na zifanyike mara kwa mara ili kuwawezesha kuwa na upeo imara na thabiti katika kulinda raia na mali zao.
  5. Mheshimiwa Rais aendelee kuwatia moyo,kuwaamini,kuwapa ujasiri ktk utendaji wao wa kazi na majukumu sawia..Hili linawaimarisha sana kisaikolojia,kimazingira,kimamlaka na heshima yao kuongezeka..
 
Hayo yote yatawezekana kama wanasiasa wakiacha kuingiza siasa mahali ambapo haihitajiki siasa
 
Back
Top Bottom