mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Hawa jamaa nawakubali nawaona kama manabii wa kweli kama zaidi ya muongo mmoja nyuma walilia sana kuhusu umeme na maji huku wakisema umeme na maji sasa ishakuwa kero kero.
Pamoja na nyimbo nyingi nyingi nzito walizowai kuimba za kimapinduzi lakini taifa halijawai kuwatambua au kuwakubali lakini unabii wao mtautambua taifa zima kuwa hawa jamaa walikuwa maprofeti.
Watafiti wa mambo ya kimazingira na majira ya vipindi vya dunia wanasema huenda hari ya ukame ikaongezeka na kuleta kero kubwa sana katika jamii kwa umeme na maji.
Kama hatua za makusudi hazitachukuliwa tutapata kero na majanga makubwa. Tayari mpaka sasa kuna mataifa mengi yanatumia maji ya bahari kwa kunjwa na kuzalisha umeme wa upepo, hizi ni nishati ambazo hazina ugonvi na mtu kama kugombeana maji ya mto Nile.
Wagosi walishauri siasa zipungue katika umeme na maji.