sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,488
Asalam Alekhu wanabodi,
Natambua uwepo wa wanaMMU wenye kutoa ushauri mzuri, kejeli, matusi, mzaha, madongo, like, bila kuwasahau wa mipasho. Itifaki imezingatiwa.
Kuna hili jambo limeshamiri kwa kiasi fulani kwenye jamii zetu ambalo kiukweli siyo zuri na ingependeza kina dada wenye tabia hizo kujitafakari, na wale ambao wana mpango wa kufanya hivyo pia wasifanye hivyo.
Unakuta mdada anazaa hata watoto 6 kila mtoto ana baba yake, na akishapata ujauzito fainali kuanzia kulea mimba hadi mtoto akue anaenda kumalizia nyumbani kwa wazazi, na mtoto akishaweza kucheza tu, anamwachia mama amtunze, yeye anaenda huko kutega tena, hadi anafikisha hata watoto 6 na unakuta bibi yao ndo anahangaika kila kitu na hao watoto hadi shule!
Hivi mdada kama huyo anafaa apewe jina gani maana siyo ustaarabu hata kidogo. Hata kama ni watoto wawili, hayo bado siyo maadili. Na sitakubaliana na anayesema baba zao wanakataa mimba, baba 6 wote wakatae mimba? Halafu kina baba hawakatai mimba bila sababu tena za msingi.
Halafu kuna mitoto mingine inaletwa kwa staili hiyo, unakuta ina mitabia ambayo unaweza ukatafuta kijiji kizima mwenye tabia hiyo asiwepo. Sote kwa pamoja tukemee kina dada wenye tabia za aina hizi. Wapo watoto sasahivi wanamaliza hata chuo kikuu na hawawajui baba zao, na sio kwamba hawapo hai, bali tatizo ni hawa dada zetu.
Nawatakia Jumapili njema wote.