Aungwe mkono kwa lipi? Kwa haya matamko ya majukwaani yasiyokuwa na Sera wala kanuni wala sheria zitakazoongoza maagizo yake? Chukua mfano wa elimu bure jinsi isivyowezekana kwa ghafla hivi. Hizo capitation zina miaka hazijafika mashuleni. Madawati na vyumba ya madarasa na vyoo hakuna. Suala LA ulinzi na madawa ya usafi wa vyoo na zana za kufundishia na kujifunzia zitachipuka tu Kama maagizo yake? Angejipa muda wa kuandaa namna ya kutekeleza na siyo kutamka na kutekeleza Kama amri ya mguu pande mguu sawa. Bado sana kwa Hays maagizo yake kutoa matunda yanayotarajiwa na wengi. Vinginevyo ajiandae kushindwa kwa kiasi kikubwa kwa eneo hili la elimu bure.