Tuwaambie tu ukweli kina dada, ni wachache mno wanaopendeza kwa suruali

Ukiweza kujibalance hapa katika suala la mavazi basi.
Screenshot_20210615-115701.jpg
 
Inashangaza kuona hadi wachungaji waumini wanajiita walokole nao wameingia kwenye huo mkumbo wa wanawake wa kidunia kuvaa suluari

Maandiko yameainisha wazi kuwa mwanamke asivae mavazi yamfaayo Mwanaume na Mwanaume asivae ya mfaayo mwanake maana ni machikizo machoni pa Mungu.
 
Ni wachache mno, wengi wao ni mkumbo tu na kufuata upepo wa fasheni. Elewa hakuna kitu kwa ajili ya kila mtu, chagua chako na ukubali. Kama ilivyo kwa wanaume, sio wote watavaa pensi.

Sketi na magauni yanawakaa poa sana, hata wale wenye maumbo ya kanda pendwa hupendeza.

Suruali sina ubaguzi. Zikigoma acha, unakuwa kituko. Tatizo watu hawatakwambia ukweli, na sio kweli kwamba hawajali eti watamaindi mambo yao.

Unajitekenya tu.

Basi sikia ushauri, au endelea kushupaza shingo ili utusaidie vichekesho vya bure tupunguze stress zetu.

Ncha Kali.

Waeleze hivi, mwanamke mwenye kitambi suruali haikfai
 
Wanawake wengi hupendeza na suruali........
Hii ni kweli but pia penda kusikiliza maoni ya ya watu wengi kuhusu mavazi yako

Mfano mimi naambiwa napendeza sana nikivaa suruali na vigauni vifupi vya kunibana tofauti na hizi nguo eti sipendezi kiviiiile

Which is true nikivaa hizo nguo full kusifiwa mpaka kero!

Kwahiyo watu ni muhimu pia kuwasikiliza

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ila tuache utani, aliyewashonea Suruali Traffic wa Kike hawatakaa wauone Uzima wa milele wa mbingu wala Ahera. Yaani ile suruali akiwa mbali na lile shati jeupe utadhani ni li katuni fulani, halafu tumbo kubwaaaa kalio hamna!

Skirt ziliwafichia mengi
 
Back
Top Bottom