Tuwaache waongezeke au tuwakemee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwaache waongezeke au tuwakemee?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by segwanga, Sep 18, 2012.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  [h=6]Ni wazi Wazanzibar wako clear kwenye ishu ya muungano,makundi yanayoupinga muungano hadharani yanazidi kuuongezeka.
  Nimekuta maneno haya hapa chini kwenye fb page ya ustaadh Ismail Jussa kuhusu muungano licha ya yeye kutanabaisha kuwa anaongelea uchaguzi wa bububu lakini lengo lake ni muungano.Msome mwenyewe hapa chini.


  [/h][h=6]"Uchaguzi mdogo wa Bububu: Mengi yamesemwa toka jana. Naziona hamaki na hasira, nazihisi hisia za kukata tamaa na kutafishika. Uchaguzi wa Bububu ulikuwa ni zaidi ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwakilishi. Haukuwa uchaguzi kati ya CUF na CCM kama wengi walivyodhania au walivyoutazama. Ulikuwa ni mfano wa kura ya maoni ndogo kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maridhiano na wayachukiao. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maendeleo na wahafidhina. Lakini kubwa zaidi ulikuwa ni uchaguzi kati ya wanaotaka Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na wale vibaraka wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa koloni la Tanganyika. Umma ulipoonekana kuwa upande wa wanaopenda maridhiano, wanaotaka maendeleo na wanaoitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, watawala wakijumuika kati ya vibaraka waliopo Zanzibar na wakoloni wanaowatumikia wakaamua kutumia nguvu kubwa ili kujaribu sauti ya nguvu hiyo isitoke.

  Wasichokijua ni sauti imetoka na imesikika, tena bila ya kisisi. Balozi Seif Ali Iddi (katika comment moja jamaa alimwita Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar) na wenziwe wanaotumikia agenda ya Tanganyika hapa Zanzibar walidhani kwa kutumia nguvu ile kubwa watatuyumbisha na kutuhamakisha tuivunje Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo yeye na wenzake hawakuahi kuiamini wala kuiunga mkono na kwa kufanya hivyo wakadhani watafanikiwa kuyavunja maridhiano na umoja wa Wazanzibari. Wakadhani wakifanikiwa katika hilo watakuwa wamevunja umoja na ari ya Wazanzibari kudai nchi yao. Wamepwerewa wao na mabwana wanaowatumikia. Akili zetu razina. Haondoki mtu kwenye mstari. Tutayalinda maridhiano na umoja wa Wazanzibari. Na tutalilinda na kulipeleka mbele vuguvugu la Wazanzibari linalojumuisha makundi na taasisi tofauti kuirudisha Zanzibar yetu".  [/h]My take
  1.Hivi maridhiano kati ya cuf na ccm Zanzibar yalikuwa kuvunja muungano?
  2.Inaonekana Zanzibar sio tu imegawanyika katika makundi makubwa mawili yaani CCM na CUF,kuna makundi mengine yanayoundwa na wanachama wa Cuf na CCM linaloitwa wanaotaka kujitenga.
  3.Kama muungano unapingwa kwa uwazi kabisa bila kupepesa macho wala kumumunya maneno na wanasiasa hasa wa CUF,Sera ya Cuf ikoje kuhusu muungano.
  4.HITIMISHO,TUWAACHE WENDELEE NA CHOCHOKO AU TUWAKEMEE? KAMA INASHINDIKANA,KUWAKEMEA,WATAZIDI KUONGEZEKA NA KWA JITIHADA HIZI WANAZO FANYA ZA KUJIANDAA KUVUNJA MUUNGANO,WATANGANYIKA ITAKULA KWETU KAMA ILIVYOKULA KWETU ILIPOVUNJIKA EAC! TAFAKARI,CHUKUA HATUA! MWABEJA SANA!
  [h=6] [/h]
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Siku CCM itatoka madarakani basi na Muungano unawafata huko waendako.
  Suali gumu kujibika ni lini CCM watatoka madarakani?

  CCM wanabaki madarakani kwa "ushindi wa kishindo" na sio kwa kuchaguliwa kwa kura!

  Muungano ni mali ya CCM na ndio walijipa jukumu la kuulinda.

  Watanganyika na wazanzibari kama wananchi wa kawaida ni wahanga tu wa CCM na muungano wao.
   
Loading...