Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,271
- 29,934
Wandugu hebu sikia hii, inaweza kutupa fundisho fulani.
Imetokea jana kwa familia ninayoifahamu vizuri huko Bukoba.
Wamezaliwa watoto 10, angalau 6 miongoni mwao wana kipato kizuri,
wanakaa ktk mikoa ya Dar, Mwanza na Mara.
Wazazi wao wanaishi ktk nyumba ya udongo kwa miaka mingi, jirani zao wote wana nyumba za kisasa na zina umeme.
Baba yao amekuwa akisononeshwa na hiyo hali, hasa kwa kuzingatia kuwa watoto wake wana uwezo kwa muda mrefu.
Mwanzoni mwa mwaka huu watoto wakaungana wakaazimia wawajengee wazazi wao nyumba nzuri, wakamtuma fundi kutoka Mwanza.
Nyumba ilikamilika Oktoba mwaka huu.
Wakakubaliana waifungue rasmi Xmas hii(jana).
Juzi wote waliwasili na familia zao, wakaanza maandalizi ya tafrija ya kuwaingiza wazazi wao kwenye nyumba ya kisasa siku inayofuata.
Ilipofika jana asubuhi mzee akawaita watoto wote kwa mazungumzo, akawaambia, "Watoto wangu nawashukuru sana kwa uamuzi mzuri wa kutujengea nyumba ya kisasa wazazi wenu.
Tunashukuru kwa kuwa mmetambua ktk eneo hili, ni sisi wazazi wenu tu tuliokuwa tumebaki kwenye nyumba ya udongo.Hata hivyo mlichokifanya kinawafurahisha nyie wenyewe, lakini siyo mimi, mama yenu wala wana kijiji wenzetu.
Baadhi yenu hapa mmekuwa na maisha mazuri kwa zaidi ya miaka kumi na tano, wakati mwingine mmekuwa mkitupeleka kwenye nyumba zenu nzuri kwa ndege, huko Dar na Mwanza.
Lakini mkasahau kuwa hata sisi huku tulihitaji kuishi kwenye makazi bora.
Angalieni umri wangu, sina mwaka mmoja zaidi wa kuishi, mwangalie mama yenu, hawezi tena kutembea.
Mimi najua, mmeona tunakaribia kufa, mkatambua kuwa rafiki zenu watakaowasindikiza kuja kutuzika watawashangaa kwa kuona sisi tunaishi kwenye nyumba duni,
Ndio maana mmejenga nyumba hii, wala sio kwamba mnatupenda bali mnakwepa aibu.
Kwa hiyo sisi hatuingii kwenye hiyo nyumba, tutabaki kwenye hii nyumba yetu ya udongo, mliyozaliwa na kukulia hadi mkapata maisha mazuri."
Baada ya maneno hayo, mzee aliwataka wabomoe hiyo nyumba mpya kwakuwa wameijenga kwenye shamba lake bila idhini yake.
Jamaa wamechanganyikiwa. Juhudi za wazee na uongozi wa kijiji kumshawishi mzee abadili msimamo wake zimegonga mwamba.
Wengine wamerudi Bukoba mjini kutafuta guest house za kulala, na wengine wameanza safari ya kurudi Dar na Mwanza, hasa waliokuja na magari yao.
Je ndo wewe sasa ungefanyaje jitambue.
Nyumba imebomolewa.