Mkomawatu
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 277
- 135
Ndugu wadau wa JF nachukua fursa hii kujitambulisha kwenu ikiwa ni mara yangu ya kwanza kutawakali katika jukwaa hili maridhawa kwa ujengaji hoja anuwai zenye lengo la kupata suluhu ya changamoto mbalimbali zinazotukabili hapa nchini na hata nje ya nchi. Baada ya salamu naanza kuelezea waraka wangu kuhusu kuhamasisha watu wenye asili ya wilaya ya Kilosa kuhakikisha wanaungana pamoja kuboresha ustawi wa wilaya hii kongwe katika historia ya nchi yetu, harakati hizo za kimaendeleo zinaweza kufanyika kwa kuanzisha jumuiya mbalimbali kwa lengo la kuwainua watu kiuchumi, kuandaa mijadala ya wazi ili kukusanya maoni ya wananchi na hata kufadhili vikundi vya vijana ili waweze kujiajiri wenyewe. Ndugu zangu nitoe rai kwa vijana wenzangu tujitose katika siasa ili kuhakikisha jimbo la Kilosa na maeneo mengine nchini yanapata viongozi bora.