Tuunde Sera ya kuindeleza miji kwa kasi, tuna mapori mengi

Black Walker

Senior Member
Oct 8, 2018
107
238
Kila naposafiri huwa najikuta nakuwa mtu wa kuumia badala ya kuifurahia safari.

Naumia kwa sababu nchi yetu kwa kiasi kikubwa ni mapori tena yanayostahili watu kuyaishi ukitoa hifadhi.

Vimji vyetu ni vidogo dogo kishenzi ambavyo gari haliwezi kumaliza hata dakika 20 umetokomea kwenye mipori hata liwe kwenye mwendo wa kawaida kabisa.

Miji ambayo imejitahidi kiasi ni Dar na Mwanza lakini sehemu nyingine sidhani.

Nashauri Taifa liweke sera au utaratibu unaolenga ukuaji wa haraka wa idadi ya watu ili tuweze kupata nguvukazi kubwa ya kujenga Taifa letu.

Binafsi sifurahishwi na kuona Taifa la miaka 60 idadi ya watu pia ikakadiriwa kufikia mln 60 maana yake ni kwamba kuna watu ambao ama kwa maksudi ni wabinafsi hawataki kuzaa wakisingizia maisha kuwa magumu, jambo hili halipaswi kuonwa kama ni la kawaida ni janga kwa Taifa.

Vipi kama wote tukiamua hivyo tafsiri yake ni kwamba itafikia hatua nchi itakosa nguvu kazi ya kuaminika halafu then iweje?

Tukiendekeza uvivu wa kuzaa ipo siku tutatafutana! Kuna mwaka utafika Taifa litatakiwa liwe na watu mln 500 lakini kwa kuwa hatutaki kuzaa kutokana na sababu zisizo za msingi litakuwa na watu mln 80.

Hii maana yake ni kwamba tutakuwa hatuitendei haki kauli isemeyo "penye wengi pana mengi". Tujifunze kwa wenzetu Wachina, Nigeria, U.S.A n.k

Unamkuta mtu wa miaka 30, 35, 40, 45 anaogopa kupata mtoto/watoto na bado anajinasibu kwamba analipenda Taifa! Mbaya zaidi unakuta baadhi wana vipato vikubwa tu lakini ubinafsi , uroho na uchoyo vimewatala wanatumbua wenyewe tu.

Mwisho nashauri tuwe watu wa kutiana moyo na kwamba Tanzania ya kesho sio yako ni ya wanao.

Kwa kuona hivyo kila mtu atapata hamu ya kupata watoto na kujikuta amelipa Taifa nguvu kazi ikiwa ni pamoja na soko la ndani linaloeleweka jambo ambalo litaweza kufanya mzunguko wa pesa kuwa mkubwa.

Leo tunapotafakari miaka 60 ya uhuru tutafakari na idadi ya nguvukazi tuliyonayo kwa kuendana na ukubwa wa nchi yetu vinahusiana?

Napendekeza baada ya miaka 100 ya uhuru Taifa liwe limefikia walau idadi ya watu milioni 400.

Nawasilisha!

Ni mimi " Blackwalker'
Mtanzania halisi.
 
Nguvu Kazi tele haitumiki kuzalisha raslimali tele zilizojaa ardhini sababu hatuna viongozi wanaofikiri.
 
Hii mada haina hualisia na chochote
Kivipi? Nishawishi kwa hoja!

Umewahi kujiuliza kwa nini % kubwa ya watu wengi wanapenda kukimbilia mijini ambako idadi ya watu ni wengi kulinganisha na vijijini?

Logic ni moja tu kwamba japo maisha huko ni magumu ila wanaamini uwepo wa fursa nyingi pia, kila kitu kinaweza kubadilishwa kuwa pesa ndo maana hadi utumbo wa kuku ni dili.
 
Kila naposafiri huwa najikuta nakuwa mtu wa kuumia badala ya kuifurahia safari.

Naumia kwa sababu nchi yetu kwa kiasi kikubwa ni mapori tena yanayostahili watu kuyaishi ukitoa hifadhi.

Vimji vyetu ni vidogo dogo kishenzi ambavyo gari haliwezi kumaliza hata dakika 20 umetokomea kwenye mipori hata liwe kwenye mwendo wa kawaida kabisa.

Miji ambayo imejitahidi kiasi ni Dar na Mwanza lakini sehemu nyingine sidhani.

Nashauri Taifa liweke sera au utaratibu unaolenga ukuaji wa haraka wa idadi ya watu ili tuweze kupata nguvukazi kubwa ya kujenga Taifa letu.

Binafsi sifurahishwi na kuona Taifa la miaka 60 idadi ya watu pia ikakadiriwa kufikia mln 60 maana yake ni kwamba kuna watu ambao ama kwa maksudi ni wabinafsi hawataki kuzaa wakisingizia maisha kuwa magumu, jambo hili halipaswi kuonwa kama ni la kawaida ni janga kwa Taifa.

Vipi kama wote tukiamua hivyo tafsiri yake ni kwamba itafikia hatua nchi itakosa nguvu kazi ya kuaminika halafu then iweje?

Tukiendekeza uvivu wa kuzaa ipo siku tutatafutana! Kuna mwaka utafika Taifa litatakiwa liwe na watu mln 500 lakini kwa kuwa hatutaki kuzaa kutokana na sababu zisizo za msingi litakuwa na watu mln 80.

Hii maana yake ni kwamba tutakuwa hatuitendei haki kauli isemeyo "penye wengi pana mengi". Tujifunze kwa wenzetu Wachina, Nigeria, U.S.A n.k

Unamkuta mtu wa miaka 30, 35, 40, 45 anaogopa kupata mtoto/watoto na bado anajinasibu kwamba analipenda Taifa! Mbaya zaidi unakuta baadhi wana vipato vikubwa tu lakini ubinafsi , uroho na uchoyo vimewatala wanatumbua wenyewe tu.

Mwisho nashauri tuwe watu wa kutiana moyo na kwamba Tanzania ya kesho sio yako ni ya wanao.

Kwa kuona hivyo kila mtu atapata hamu ya kupata watoto na kujikuta amelipa Taifa nguvu kazi ikiwa ni pamoja na soko la ndani linaloeleweka jambo ambalo litaweza kufanya mzunguko wa pesa kuwa mkubwa.

Leo tunapotafakari miaka 60 ya uhuru tutafakari na idadi ya nguvukazi tuliyonayo kwa kuendana na ukubwa wa nchi yetu vinahusiana?

Napendekeza baada ya miaka 100 ya uhuru Taifa liwe limefikia walau idadi ya watu milioni 400.

Nawasilisha!

Ni mimi " Blackwalker'
Mtanzania halisi.

Kwanza tuanze na wewe, Wewe unao wake wangapi na watoto wangapi??!!----- sio kuongea tu wakati maongezi na vitendo haviendani ! !😨
 
Back
Top Bottom