GreenHouse
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 280
- 262
Wana JF wenzangu,
Leo nimeamua kuwapa habari njema kabisa katika uvumbuzi niliokuja nao... (Well Sija invent kitu hapa).
Tunaweza Kutumia Mtandao wa YOUTUBE (Thanks to google) kujikomboa na maisha yetu na kuongeza kipato au hazina yetu ya chakula...
Ni dhahiri kwamba maisha yamekuwa ghali na magumu na kila kukicha tunapanga foleni "mabenki" Kuomba mikopo na kujaribu kufanya hiki na kile, lakini Hata tukope Bilioni Ngapi, Au tuwe na mishahara mikubwa kiasi gani... Bado wimbi la umasikini Africa na Expecially Tanzania Halitoisha.... Kwasababu tu "HATUJAAMUA KUBADILIKA"
Kubadilika huku ni kupi? Tuanze sasa kupunguza gharama za maisha kwa kuzalisha na kubuni mbinu mbadala za kufungua wallet au mapochi yetu kila siku... hapa namaanisha Tuanze kufanya "Cuts" kwenye matumizi yetu ya kila siku...
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijaribu hiki na kile na kupanga budget kila mwezi na kujikuta naenda "well over budget" Kwakuwa tu, matatizo ya Africa Hayaishi, Kama si yako basi ya Extended Families, au marafiki...Na kwakuwa tumeumbwa na mioyo ya ukarimu basi tunafungua "vibubu" vyetu na kuwapa wale wenye kuhitaji, Wengine wanatutia ndani, wengine wanarudisha wapendavyo... mf: unamkopesha mtu laki tatu tu, lakini kila mkionana anakupa elf 15, mara 29 mara 50 mpaka deni linaisha, na mwisho wa siku unaishia kuwa huna ile laki 3 na humdai tena mdeni wako...
Sasa Yote haya yanaweza kupungua au kuondoka kabisa kama tunaamua kuitumia "YOUTUBE" Vema kwa kujifunza na kujielimisha katika mbinu mbali mbali za kujikimu kimaisha... Mfano mzuri tu, ni pale nilipoamua kulima kibiashara huku nikiwa sina hata mbinu moja ya kufanya hivyo... Na Kosa kubwa tulifanyalo ni kununua mashamba, unajenga kibanda na kumuweka kijana shambani, halafu yeye ndio anakuwa mtaalamu wako sasa wa kilimo... Yaani ukitaka kulima nyanya, unaenda shamba, sasa Bwana fulani, leo nataka tulime nyanya hapa, tunafanyaje... na yeye kwa kujigamba kabisa (hata La Saba hakumaliza) Anakwambia Mzee hapa mbona nyanya zinatoka kabisa, tena tunavuna kweli kweli, haya unampa jembe anaanza kulima kibustani, anakimwagia ukiwa unataka kwenda siku usipokuwepo kinakauka na jua.... Anarundika mimbolea na madudu gani sijui... mwishowe hupati kitu, una "CONCLUDE" Aah Kilimo Hakilipi bwana, bustani hazina maana... Unaenda bank unakopa pesa unanunua dala dala, madereva wanakuibiaa weeee, unauza unahamia kwenye kitu kingine...
Hivi tumeshawahi kujiuliza kwanini tunaanzisha miradi na kila siku inakufa au tunafunga maduka na madeni yanaendelea kama kawaida??? JIBU NI MOJA TU.... HATUJIFUNZI.. Yaani HATUSOMI UTAALAMU WA KUENDESHA MIRADI YETU... Biashara zetu zinaendeshwa na wasiosoma, wasiomaliza hata form four... Tunawapangia hesabu au mikwala mingi na hatupati kitu, mwisho wa siku tunaishia kuanguka na miaka inaenda mahitaji yanakuwa na tunakufa masikini....
YOUTUBE ni mtandao wa bure kabisa ambao ukitaka kusoma kweli utapata utaalamu wa hali ya juu mpaka unashangaa...
Mimi nimeamua kuanzisha Kilimo cha miti ya matunda na nimeapa kuwa sitotumia gharama kubwa kufanikisha hili. hivyo basi nimeanza kampeni ya kushinda youtube na kusoma jinsi ya kulima, limao, ndimu, nyanya, pilipili, miembe, parachichi, na matunda mengine mengi sana,.... Guess What!!! Nimeanza kufanikiwa... Nimeshajifunza mbinu za kuzalisha miche, kuihamishia shambani, kuihudumia nk nk, na sasa natenda kwa vitendo kabisa... Ntakuwa nikiwapa updates mradi unavyoenda...
Tupunguze gharama za maisha kwa kupanda mboga mboga nyumbani hata kwenye makopo, kwani wengine hawajajaliwa kujenga na kuwa na maeneo ya bustani nyumbani... Nyanya, pilipili hoho, mchicha, ndimu nk, sio lazima vilimwe kwenye ardhi kubwa....
Nimeshawahi kupanda mnyanya mmoja na nikavuna nyanya za kupikia kila siku kwa muda wa miezi miwili....Niliufunga kamba mpaka juu ya bati, kila siku nikawa nachuma nyanya tatu nne tunapika tunakula.... Nina minazi mitatu nyumbani, na sijanunua nazi zaidi ya miaka miwili sasa, naita kijana anapanda na kuangua nazi 30 kwa mara moja zinapikiwa mwezi mzima, sasa nimeanzisha kampeni ya kupanda miche ya minazi mwenyewe nyumbani niihamishia kwenye lile shamba langu la miti ya matunda....
We ingia tu youtube halafu andika how to grow tomatoes at home, uone ni videos ngapi zitakuja, au aundiaka how to plant lemon from seed nk...
Nyanya, ndimu, limao, machungwa na vinginevyo tunavyokula kila siku na kutupa mbegu hovyo ndio hizo hizo tunazoenda magengeni kuzinunua kwa bei kubwa na tunasema maisha magumu wakati tungepanda nyumbani, tusingeingia gharama ya kuzinunua....
KILIMO NI UJUZI Jamani, tujifunze japo kuhudumia bustani za mita tatu nyumbani kwa chakula chetu wenyewe... tutaepukana na kununua fungu la mchicha kwa 500, nyanya moja 100, bamia nne mia mbili nk.... Kama TESCO Wanavyosema... "EVERY LITTLE HELPS"...
Nisiwachoshe kwa uzi mrefu ila nadhani mmenipata...
Niwaache na video hii ya upandaji nyanya nyumbani ....

Last edited by a moderator: