Tutumie hili la Urusi na Ukraine kujijenga.

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Vitu vimepanda bei, serikali inajaribu kustablize mambo, raia wamecharuka lakini ukweli wa mambo huwezi kuwa na power ya kubargain kama huna kitu.
Kama taifa tumekaa tunasubiri Urusi na Ukraine wamalizane ili tushishiwe bei ya ngano na mafuta ya kupikia.
Kwanini tusiwaze mbele zaidi? Magufuli baada ya changamoto ya sukari kila mwaka akaona ampe Bakhresa eneo la kulima miwa na kuzalisha sukari. Kwa kile kiwanda kinavyoendelea naiona bei ya sukari ikishuka na kuwa stable?
Kwanini hilo tusilifanye kwenye ngano, alizeti, ufuta na mawese?
Kuna vitu tutaimport lakini tuweke mikakati tusiimport mazao yoyote kwani tuna ardhi kubwa nguvu kazi na uwezo wa kulima wenyewe.
Tuimport magari lakini sio mafuta, tunazungukwa na nchi zenye changamoto ya vyakula na mazao.
Kwanini tusiongeze nguvu kwenye uzalishaji wa mazao za biashara na chakula?
Kwanza tutapata ajira, tutapata fedha na kutapunguza njaa za kijinga kwa mataifa mengine.
Kilimo tu ndo kitatutoa, tufanye kilimo cha kisasa tuweke nguvu ya kutosha kwenye vipaumbele vichache, tukipe promo kama ya "kilimo kwanza" tukipe uzito sana naamini tutatoboza.
Bashe anafanya vizuri hadi sasa naamini akiongezewa support anaweza kufanya transformation kubwa.
 
Back
Top Bottom