chongoe
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,221
- 2,971
Ilikuwa siku moja upepo mkali sana baharini hakuingiliki; hatuwezi kusafiri sababu upepo ulikuwa mkali. Sasa ikawa sina ujanja, nasubiria bahari itulie tuanze safari.
Bahati mbaya ilichukua siku nne bahari kutulia na mfukoni sina kitu. Mida ya asubuhi naelekea zangu beach nikafanye mipango ya pesa angalau nipate kitu sababu baharini sijui lini itatulia, kabla sijafika beach, nikakutana na msafara wa magari umebeba maiti.
Ikabidi nisimame pembeni ya barabara; ndio sharia kwa Waislam. Lakini muda huo nawaza nitakula nini maana siku ya nne hali yangu ngumu, nakula ila kwa kudoeadoea.
Mara ghafla ile gari ilienda kusimama kwa mbele, kuna jamaa aliteremka akaja. Kumbe namfahamu na yeye anifahamu; tulisoma wote Tanga. Baada ya kunifikia akaniambia twende kwenye gari tupeleke maiti ikaoshwe. Wakati anasema hayo, mimi nawaza beach kwanza nikaangalie jahazi usalama wake. Jingine, hali yangu kifedha ngumu ikabidi nimwambie yule jamaa. Akasema we twende wala usijali, basi nikapanda ndani ya gari mpka unapofanyika msiba tukateremsha maiti.
Yaani muda huo mimi nina njaa kinoma, alafu ni asubuhi hiyo. Baada ya kuteremsha ikaingizwa ndani. Baada ya muda yule jamaa akaniita na kuniambia akasema itabidi Mimi nioshe maiti. Sikuwakatalia kuosha; ila kutokana na kazi yangu ya bahari, kuosha maiti ni kama uchuro. Baadae ntawaeleza kwanini inakuwa uchuro sisi kuosha maiti.
Wenye maiti walinambia watanipa 25000 Baada ya kuwaoshea maiti yao. Sasa wakati naingia chumbani nikasikia jina langu linaitwa ikabidi nirudi kuangalia nani ananiita. Alikuwa mtu mzima wastani tu; akanisalimia pale mbele za watu kama vile twajuana kumbe wala simjui. Akaniambia samahani kwa muda wako, nisaidie jambo nitakupa pesa. Nikamuuliza jambo gani, akaniambia yeye amepata khabari kuwa mimi ndio ntaenda kuosha maiti kwahiyo akanambia: "Naomba utapoenda kuosha maiti mimi nachohitaji ni maji ya maiti na kipande kidogo cha kitambaa ambacho hufunikiwa maiti kwa ajili ya kuoshea"
Pia kasema nakupa laki moja; ntakukabidhi hapo hapo baada ya kumaliza.
Nitaendelea wadau. Hiki kisa kisa kirefu sana.
Samahani kwa muandiko mbovu. Mimi nahodha tu