Tutavuna tunachokipanda

Tutavuna tunachokipanda

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Jana taasisi ya utafiti ya TWAWEZA ilitoa utafiti kuhusu sauti za wananchi katika swala la Elimu nchini.

Katika utafiti wao wananchi wamechagua kuchangia Elimu ya Watoto wao alimradi tu iwe bora. Swali likiulizwa ni kigezo gani hutumia wakati wa kumchagulia mwanao shule ya Kujiunga nayo kidato cha kwanza? Majibu yakikuwa kama yafuatayo.

1. Asilimia 72% walidai watachagua shule yenye waalimu wenye morali ya kufanya kazi.

2. Asilimia nyingine 72% walidai Watachagua shule yenye ufaulu mzuri kidato cha NNE.

3. Asilimia 54% wakasema watachagua shule yenye miundombinu mizuri.

4. Asilimia 6% ndio walichagua ada kidogo.

Tafsiri yake ni kuwa watu wapo tayari kushirikiana na serikali katika kuboresha ubora wa Elimu Tanzania. Niliwahi kusema kwa Wenzetu Kenya wana kitu kinaitwa Private, Public Partnership kwenye elimu ambapo ni fursa kwa wazazi kuchangia katika elimu ili kuboresha zaidi fungu linatolewa na Serikali.

Nafikiri kila mtu ni shahidi jinsi watu wengi wanavyojitokeza kuchukua Form za kujiunga kwenye shule za Private zinazofanya vizuri kwenye matokeo ya Kidato cha nne. Shule hizi hazijawahi kukosa wanafunzi badala yake huzidiwa na wanafunzi.

TAFITI ZINAONYESHA WASIOMUDU KKK WANAZIDI KUONGEZEKA.

Mapema mwaka huu mwezi wa pili taasisi ya maswala ya utafiti ya UWEZO ilitoa ripoti yake ya utafiti ulioendeshwa mwishoni mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

Utafiti huo ulilenga kupima uwezo wa wanafunzi katika stadi za kusoma kuhesabu na kuandika. Katika utafiti wao wanafunzi wenye umri wa miaka 9-13 walikuwa ndio walengwa.

Kitaalamu mtoto huanza la Kwanza akiwa na miaka Mitano hadi miaka 6 kwa maana hiyo mtoto mwenye miaka 9 tunamkadiria kuwa darasa la tatu kama alianza shule na miaka sita huku miaka 10 akiwa la nne, miaka 11 akiwa la tano na miaka 12 atakuwa la sita na miaka 13 ambayo ndiyo ilikuwa limit ya mtafiti akiwa la Saba.

Wanafunzi hawa walipewa majaribio ya mtihani wa darasa la pili. Yaani tunasema sample ilijumuisha wanafunzi kuanzia la tatu hadi la saba na walipewa mtihani wa darasa la pili.

MATOKEO

Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 88 ya wanafunzi waliopimwa hawakuweza kufanya maswali hayo ya darasa la Pili.

Utafiti umebaini pia kwamba Maeneo ya pembezoni mwa nchi tatizo ni kubwa sana.

Kwa mfano kwenye utafiti wanadai kuwa asilimia 75 walioweza maswali hayo ya darasa la pili walitokea wilaya ya Iringa mjini wakati maswali hayo hayo kwa wanafunzi wa wilaya ya Sikonge walioweza ni aslimia 17 tu.

Kwa tafsiri Rahisi ni kwamba katika sample yao yote ya utafiti asilimia 12 tu ndio waliomudu majaribio hayo ya darasa la pili huku asilima 88 wakishindwa. Hiyo asilimia 12 iliyoweza asilimia sabini na tano yake wanatokea Iringa mjini na asilimia 17 inatokea Sikonge.

Mwaka 2010 ripoti ya utafiti ya Uwezo ilikuja na matokeo kuwa kati ya wahitimu 5 wa darasa la saba Mmoja wao alikuwa hajui kusoma kabisa sentesi Rahisi ya darasa la kwanza. Katika ripoti hiyo ilionyesha asilimia 42 tu ya wahitimu hao ndio waliokuwa wanaweza kusoma kwa ufasaha.

Mwaka 2014 taasisi ya uwezo ilikuja na ripoti nyinginine na kuonyesha kuwa Watoto wanaotokea familia Maskini kati ya asilimia 100 ya waliokuwepo kwenye utafiti ni asilimia 40 tu walioweza kumidu Stadi za KKK. Kwenye ripoti hiyo ya Uwezo wanaonyesha kuwa watoto wanaotokea familia tajiri wana uwezo mkubwa zaidi wa kumudu stadi za KKK kwani katika asilimia 100 wao asilimia 60 wanamudu stadi hizo.

TAFITI HIZI ZINATUAMBIA NINI?

Toka mwaka 2010 tafiti zinatoka na inaonekana tupo pale pale. Ni kama vile hatusogei badala ya Kusogea tunarudi Nyuma.

Tafiti hizi zinaonyesha kuwa watoto wanaotokea familia za Kimaskini wanaathirika zaidi na Mfumo wetu wa Elimu tulionao.

Kama juhudi zisipochukuliwa idadi ya wasiojua kusoma na kuandika itaongezeka siku za usoni.

Sijui tunakwama wapi ila Swala la Elimu Tanzania linahitaji mjadala mzito wa wanataaluma na Sio wanasiasa.

Maoni yangu ... elimu ya awali ipewe kipaumbele kwani ndio msingi wa elimu kwa watoto wetu. Sisi Mwasenda Development Intervention (NGO) tumejikita zaidi kwenye kutoa elimu ya awali kwa watoto wenye umri chini ya miaka saba. Tunahakikisha watoto hawa wanakuwa na uwezo wa kuujibu maswali hata ya darasa la pili.

Natoa wito kwa wazazi, shirikianeni na watoa elimu ya awali ili watoto wetu wawe na msingi mzuri. Pia watoa elimu ya awali jifunzeni kutumia Computer na hasa Internet kwani kwenye internet kuna mambo mengi ya kuwasaidia watoto wetu; kuna vitabu vya kila aina na vinapatikana bure.
 
Jiwe linawacheki tu pembeni kisha lasema... ' ihiiiiiiiiiiiiiii'...
 
Back
Top Bottom