Henry Philip
Senior Member
- Jul 29, 2008
- 113
- 32
Natumaini kuwa kila mmoja wenu ni mzima kwa mapenzi yake mola. Tunamshukuru kwa hilo.
Leo naomba niwashirikishe mada moja muhimu ambayo ni sisi tu wadau na wenye uchungu na nchi hii tunaweza kuyafanyia marekebisho kwani inaonekana kuwa viongozi tulionao na vyombo tulivyonavyo vimeshindwa kabisa katika hili.
Mada yangu ni kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta yaani petroli, diseli na mafuta ya taa. kwa kweli naomba niwe mkweli kuwa watanzania wanaumia na wanaumizwa sana ila tunavumilia tu maumivu lakini siku yakizidi ndio tutajua kuwa hali si nzuri. Naomba tu nizungumzie kuhusu mafuta ya taa. kwa sasa lita inauzwa kwa shs 950 hadi 1000 kutoka bei ya awali ya 700 kwa lita. Hivi hawa wenye matumbo makubwa watendelea kutuumiza hadi lini? na sisi tutaendelea kuvumilia hadi lini tukiangalia mambo haya yakiendelea bila mpangilio hadi lini? nikijaribu kufikiria mambo lukuki yanavyoendeshwa nchini hapa naumia sana. Hebu tuangalia maisha ya mtu wa kawaida asiye na uwezo wa kulipia umeme au gesi kwa ajili ya nishati ya kupikia kwa mfano. kwa ujumla watanzania walio wengi tunatumia nishati ya kuni, mkaa au mafuta ya taa. Sasa hawa wasio na akili timamu wanazungumza kila siku kuhusu utunzaji wa mazingira. Lakini wanashindwa kutambua kuwa kupanda kwa nishati ya mafuta ndio inachangia hasa ukataji wa miti/misitu na uchomaji wa mkaa. Hivi elimu walionayo hawa tuliowapa dhamana ya kutetea maslahi yetu ni halali kweli au ndio tuseme kila mtu chukua chako mapema bila kujali jamii iliyokuzunguka? Ni hivi majuzi tu nilisoma kwenye chombo kimoja cha habari kuwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia imeshuka kwa 3%. Kwa hili nilitegemea kabisa vyombo husika hapa nchini vingeona hili na kudhibiti ushushwaji wa bei kulingana na takwimu hizi.
Mimi ninachoomba na naomba tuungane pamoja katika hili kuwa ni wakati sasa kwa serikali hii kuacha mara moja na tunaitaka iache mara moja ushenzi huu,tumechoka sana na itambulike tu kuwa kama hali itaendelea kama hivi tutajikuta siku moja tena si mbali katika hali zilizopitia nchi kama Rwanda, Burundi, Siera leon n.k. Siwatishi ila ukweli ndio huu.
Tunaona kila siku bei ya vitu vinapanda bila mpangilio wowote na tunanyamaza tu. It will reach a time when nobody will keep quiet on this. Tuko kama tunaburuzwa kama gunia. Hakika nawaambia hali si shwari. jaribu kupita mitaani uone maisha ya watu yalivyo mabaya. Pita uone magunia kwa magunia ya mikaa yanayoshushwa kutoka vijijini. Hivi huko nako kuko salama kwa hali hii? Vyanzo vya maji viko salam kweli? Mgao wa umeme nchi hii utaisha kweli na utapeli wa akina richard monduli utaisha kweli? je ushenzi wa kuambiwa mabwawa yamepungua au yamekauka maji utaisha kweli? je bili za umeme nchi hii zitashuka kweli ili kuleta unafuu kwa watu wa hali ya chini na kuchochea kukua kwa uchumi wetu uliochoka vilivyo? Mimi nafikiri niwaaachie maswali haya nanyi muyatafakari muone tunapoelekea.
Walioko madarakani wanapiga mbiu ya kilimo kwanza kwa kuwapelekea wakulima matrekta n.k. ilhali bei ya mafuta haidhibitiwi. HUU NI UNAFKI MKUBWA SANA KWA WATANZANI NA SIONI NIA YA KWELI KATIKA HILI.
Imekuwa ni kama kasumba kuwa bidhaa ikipanda bei nchi hii ni mpaka wananchi wapige kelele sana na vyombo vyenye uchungu na nchi hii ndio HAWA WEZI wanaogopa na kujaribu kufuatilia. Mfano mdogo tu ni hivi karibuni bei ya vocha za simu zilipanda from nowhere. Kama si wenye uchungu na nchi hii kupiga kelele vilivyo hakika tungekuwa tunakiona cha mtema makuni.
KWA KIFUPI "THIS IS THE TIME THAT WE NEED A TRUE LEADER WITH CLEAR VISION" Naomba tuamke pamoja la sivyo tutabakia kila siku kusema ooo nchi fulani mwaka fulani tulikuwa nayo sawa kiuchumi, na watoto na wajukuu wetu watarithi hili na miaka nenda miaka rudi tutabakia hivihivi>
Gob bless all of you.