Tutarajie taifa bovu lenye viongozi wabovu:MWANANCHI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutarajie taifa bovu lenye viongozi wabovu:MWANANCHI

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 25, 2010.

?

SHERIA YA UCHAGUZI INACHANGIA KUTAMBA KWA UONGOZI MBOVU?

 1. HAPANA UMASIKINI WETU NI LAANA TU!

  0 vote(s)
  0.0%
 2. HAPANA MBONA MAMBO NI SWAFI CHINI YA HIMAYA YA CCM?

  0 vote(s)
  0.0%
 3. *

  NDIYO UMASIKINI NI UTHIBITISHO WA UONGOZI BALAA

  100.0%
 4. SIJUI!

  0 vote(s)
  0.0%
 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  Tutarajie taifa bovu lenye viongozi wabovu Send to a friend Tuesday, 07 September 2010 17:19 0diggsdigg0diggsdigg  Na Anthony Mayunga

  TANZANIA ni nchi ya kwanza kutekeleza azimio la nchi wanachama wa SADC la kutunga Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
  Azimio hilo la umoja wa Afrika lililopitishwa katika mkutano uliofanyika Maputo julai 2003, ambalo lilizitaka nchi zote wanachama kutunga Sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha kipindi cha Uchaguzi.
  Sheria hiyo Namba 6/2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Februari 11 na Machi 17, 2010 Rais Jakaya Kikwete alisaini sheria hiyo ili iweze kutumika.
  Alisaini kwa mbwembwe nyingi tena hadharani, huku akijinasibu kwa maneno ya kujiamini kuwa hiyo ni mwarobaini wa wanaosaka uwakilishi, uongozi kwa njia ya rushwa.
  Lengo likiwa ni kudhibiti matumizi ya fedha za gharama za uchaguzi, kuzuia vitendo vya rushwa, kuweka mipaka ya matumizi ya fedha na gharama zinazotumika katika mchakato mzima wa uteuzi, kampeni na uchaguzi.
  Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa wasaidizi wake,na wabunge wa CCM ambao kwa kauli moja Februari 11 mwaka huu Spika alipouliza,”mswaada huu upite, wakaitika ndiyooooo wangemsaidia wakati wa utekelezaji.
  Kutoka kwa wabunge wachache ambao wanadaiwa wa upinzani ilisikika hapana kwa kuwa walishaona mapungufu ya Sheria hiyo wakati wa utelekezaji, zaidi ililenga kubana wapinzani na wale wapya wanaotaka nafasi za uwakilishi.
  Lakini ni mambo yasiyohitaji wasomi kujua kuwa wanaoongoza kwa kukiuka Sheria hiyo siku chache tu baada ya kupitishwa ni wale walioitikia ndiyoooooo.
  Na ni jambo la kusikitisha kabisa kuona wale wanaotakiwa kumsaidia Rais Kikwete ndio wanaoongoza kwa kutoa rushwa ya fedha na vitu mbalimbali ili waweze kuchaguliwa kuanzia mchakato wa kura za maoni CCM.
  Wanaofanya hayo ndio wanategemewa kuteuliwa kuwa Mawaziri katika serikali ya awamu ya nne ambayo imeshajipambanua kwa mikakati mingi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
  Kutokana na faulo wanazocheza sasa kwa kutoa rushwa hadharani, na ni hawa hawa watakaohusika kusaini mikataba mbalimbali ndani na nje ya nchi.
  Hivi kweli watakuwa wasafi mara baada ya kuteuliwa kuwa mawaziri, kama sasa wanaongoza kwa kutoa rushwa ili wawakilishe wananchi ambao walitakiwa kumgharamia wanayemtaka si mwakilishi kuwagharamia anaotaka kuwawakilisha.
  Miaka mitano iliyopita tumeshuhudia mikataba mingi mibovu ya kukamua Watanzania hadi damu, waliohusika baadhi sasa hivi wanatapanya pesa walizochuma ili waweze kuchaguliwa tena, nashawishika kusema hali yetu ni ngumu sana.
  Licha ya kuwapo kwa Sheria hiyo iliyopitishwa haraka haraka, tunashuhudia kuwa watendaji na watoa maamuzi katika serikali yetu hawana Uwazi katika uwajibikaji.
  Maana haiwezekani kuwapata Mawaziri wanaozingatia utawala bora unaohusu kuhodhi madaraka, ikiwa ni njia ya kuendesha serikali, taasisi kwa kuzingatia viashiria vya utawala bora kutoka kundi hilo ambalo limepagawa kusaka madaraka kwa gharama yoyote.
  Haiwezekani watoa rushwa wabadilike na baadaye waweze kuzingatia uwajibikaji, uwazi na kuwa na ufanisi katika utendaji na utoaji huduma, uongozi ulio adilifu wenye hekima na uangalifu na uadilifu katika matumizi ya nyenzo na rasilimali za serikali. Kwa kuwa hawaja wa kweli kwa wananchi wanaowachagua haiwezekani wawe wakweli, waaminifu na wawajibikaji kwa matendo yao. tutaraji taifa bovu lenye viongozi wabovu kama tutaendelea na kuwa na mfumo wa waziri lazima awe mbunge.
  Maana kwa faulo wanazocheza sasa hadharani, huku wengine wakiogopwa na Takukuru, wamefikia hatua ya kudharau demokrasia ya kweli iliyopo kwa manufaa ya wote.
  Tulitegemea CCM ingekuwa kinara cha kuenzi kila wanachokipitisha kwa sauti moja kuu ya ndiyoo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha demokrasia ambayo inabainisha wazi kuwa viongozi wanatakiwa wapatikane kwa njia iliyo huru na haki.
  Njia ambayo inawapa wananchi kupima utendaji wa walioko madarakani au watawala, badala yake wanaonekana wala na watoa rushwa. Rushwa hukosesha uaminifu, husababisha dhuluma, ubovu katika menejimenti ya taasisi au nchi.
  Kupata madaraka si kwa mtindo ambao unaendelea wa kutoa fedha huku wananchi wanaowataka wawachague wakiwa hawapati huduma za jamii, watoto katika majimbo yao wanakaa chini,vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano vinaongezeka.
  Ni hawa hawa wamekuwa wakijinadi kuwa ilani ya CCM imetekelezwa, sasa rushwa ya nini kama wananchi wamehudumiwa vema. Kwa ujumla ni aibu kubwa kwa serikali iliyoko madarakani, maana hata
  wakuu wa wilaya, mikoa na kila aliye na madaraka aliyejitokeza kugombea amekuwa tatizo kwa utoaji rushwa.
  Hivyo kutokana na vitendo vinavyoendelea baadhi ya makamanda wa Takukuru wamekuwa kimya, wakishuhudia wagombea hasa wale vigogo wakigawa fedha hadharani.
  Wananchi watashangaa kuona watu hao hata kama watashinda wakaachwa kuendelea kugombea nafasi hizo, maana matumaini ya wananchi ni kuona watuhumiwa kama hao wanaenguliwa hapo wataamini kuwa sheria hiyo haikuwa kwa ajili ya wadogo kama inavyosemekana.
  Maana kuwaacha watu hao ni kutengeneza taifa bovu lenye kujawa na mafisadi wakubwa ambao hawatakuwa na nia thabiti ya kupambana na maadui watatu wanaosumbua wananchi, ujinga, maradhi na umaskini wa jamii bali wa familia zao ili kurudisha fedha walizotumia.
  Wapo wanaosaka nafasi hizo umri wao umeenda hivyo watakachokifanya ni kujikusanyia fedha waweze kumaliza wakiwa na uchumi mzuri na hawataweza kuwawakilisha vema wananchi ikizingatiwa kuwa walitumia mamilioni ya fedha kutafuta uwakilishi.
  Vitendo hivyo ni pigo kubwa kwa CCM ambayo inatamba kuwa ni chama makini lakini chenye wanachama wasio makini, waadilifu, maana haitarajiwi kuona watu wanaotaka kwenda kutekeleza Ilani iliyokwisha wekwa hadharani kwa utoaji rushwa namna hiyo.
  CCM wakumbuke kuwa matatizo ya nchi hii wameyatengeneza wao na huenda kwa makusudi ili kundi kubwa liendelee kuwa omba omba, linalosubiri Sh1000, chumvi, khanga, fulana kwa miaka mitano.
  Naamini kuwa CCM kama itataka kuinusuru nchi hii mikononi mwa mafisadi, wale wote waliobainika kumwaga rushwa wasipewe nafasi ya kuwawakilisha wananchi.
  Waachwe tena hata ndani ya chama wasipewe nafasi maana wamekosa uadilifu, hawafai katika jamii, kuwatesa wananchi kwa kukosa hata chakula kwa kila siku wao wanapora fedha ambazo wanakuja kuzimwaga wakati kama huu.
  Kikwete kumbuka, akili za kuambiwa ongeza na za kwako, chama kitakufia kama utaendekeza kuwa na viongozi wa aina hii ambao wanaua Watanzania ili kupata madaraka.
   
Loading...