Tutarajie kuwaona nyoka wengi majira ya mpukutiko lakini tusiwaue tufahamu namna ya kuwa handle

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
442
1,011
Kuna baadhi ya watu wanasema nyoka mzuri pekee ni nyoka aliyekufa lakini wataalamu wanasema msemo huo upo mbali na ukweli.Wanasema uwaache sababu kuwaua utasababisha walete madhara makubwa.

Hatushauriwi kuwaua nyoka sababu nyoka wana faida kubwa kwenye eco system. Wanakula wadudu na wanyama waharibifu kama panya na wengineo ambao huleta usumbufu majumbani na mashambani.

Nyoka huonekana sana majira ya mapukutiko lakini tufahamu nyoka hawapo kutuumiza "hakuna nyoka ajitokezaye kwa nia ya kumdhuru MTU" ,watu wanakuwa na hasira tu pindi wakiwaona nyoka au wakitaka kuwaondosha.kama wameingia nyumbani kwako chukua ufagio mkubwa na kisha muingize nyoka huyo kwenye ndoo au chombo chochote aina ya ndoo na kisha mtoe nje aende zake sehemu zingine salama.

Na kama nyoka aliyeingia ni mkubwa na anasifa ya kuwa na sumu unashauriwa kuwaita wataalamu waje kumuondoa kama hauna ujuzi wa kuwakamata na kuwaondoa.Kujaribu kumshambulia utaweza kusababisha madhara makubwa kwako wewe na kwa nyoka na pia ni illegal kwa sheria za nchi kuwaua nyoka sababu wapo chini ya Mali asili na utalii.

Inabidi tufanye utafiti kufahamu aina za nyoka ,venomous snakes na non venomous snakes. Venomous snakes huwa na sifa zifuatazo:

-venomous snakes wana fangs

Pia venomous snakes wana mboni ya macho yanayofanana na paka tofauti na non venomous snakes.

79c6673ec463260aec5b230c14f7a98c.jpg


Tofauti kati ya nyoka wenye sumu na wasio na sumu kwa msaada wa picha


Non venomous snakes akikungata utahisi kujikuna na hawana fangs ,hata nyoka wenye sumu wakikungata nafasi ya wewe kufa ni ndogo sababu ya dawa za kisasa kuwepo,pia baadhi ya venomous snakes wakikugonga hawamwagi sumu au wana venom chache ya kumuua mtu aliye na afya nzuri.

Nyoka hupenda kujificha sehemu zenye mbao nyingi ,dari zilizorundikana hata kwenye kuni nyingi sababu sehemu hizo ni nzuri kwao kujificha hivyo ni vizuri kusafisha maeneo yaliyo na mrundiko wa mbao,dari,kuni nk kuepusha kujenga makazi ya nyoka.

Nyoka wanapenda kujificha sababu wanawaogopa watu zaidi ya sisi tunavyowaogopa na endapo ukimuona nyoka rudi nyuma na tathmini hali ya hiyo sehemu.

Mwisho ukimwona nyoka relax ,kuwa calm sababu nyoka wanamuogopa mtu kuliko mtu anavyomuogopa nyoka ,Fanya experiment moja ukimuona nyoka yeyote yule hata py thon jaribu kama unamfuata /kumkimbiza atakimbia spidi kutafuta sehemu salama ya kwenda hata cobra na black mamba hivyo hivyo hukimbia lakini angalizo kama ikifika mahala hawana sehemu ya kwenda au kujificha huwa aggressive kujilinda kwa kurudisha kichwa nyuma kukuvizia kufanya strike kama hauna utaalamu mwache ondoka zako.

Kwa pamoja tulinde Mali asili zetu na tusiwaue kwa ukatili wanyama hawa

c3cf07f6c36e4cf25bbacc36348ab805.jpg



9dbb3aa78e371fd1ca007abe7fc1e9e0.jpg
 
Na kama nyoka aliyeingia ni mkubwa na anasifa ya kuwa na sumu unashauriwa kuwaita wataalamu waje kumuondoa kama hauna ujuzi wa kuwakamata na kuwaondoa.Kujaribu kumshambulia utaweza kusababisha madhara makubwa kwako wewe na kwa nyoka na pia ni illegal kwa sheria za nchi kuwaua nyoka sababu wapo chini ya Mali asili na utalii.


Hao wataalamu umewaandaa? wako wapi? weka namba zao za simu hapa eneo letu tunaua nyoka kila siku ni wengi na hawaishi
 
Dawa ya kuwakimbiza ni mafuta ya taa au kuchoma mpira wa matairi ya vyombo vya usafiri. Au kwa kisasa zaidi kufanya fumigation.
 
mkuu nyoka sumu yake ndiyo inayomsaidia kupata msosi kama vile panya kwa kuwadunga na wakapoteza fahamu.siyo rahisi nyoka kutoa hiim sumu kwa kitu ambacho hakimpi faida katu.Ukiona kakugonga ujue hakuna jinsi anajihami.
Hapo hata hujanishawishi nyoka hata enzi za Adamu na Hawa walipondwa vichwa. Au kwa vile kulikuwa hakuna slogan ya maliasili? Kuna nyoka alitoka atokako akamgonga mwalimu mmoja alikuwa anasukwa hakumaliza masaa 2. Hiyo ndiyo maliasili ya kulinda?
nyoka
 
Imezoeleka kwamba mtu atakayemuua nyoka basi huonekana ni shujaa...
Yaani ile hali nyomi ya watu imejaa huku wengine wakimiminika kuja eneo nyoka alipouwawa alafu mzee mzima ndo umesimama unaelezea ilivyokuwa mpaka ukamuua.. Huku watu wengine wakikupongeza aisee unajihisi bonge moja la shujaaa...
 
Back
Top Bottom