Tutakukumbuka kwa lipi?

Faru John II

Senior Member
Dec 27, 2016
134
135
Karibu asilimia 90% ya watu wanaokufa hufa ilhali wakiwa katika masikitiko na majuto makubwa sana.

Sababu kubwa inayowafanya watu hao kuwa katika hali hiyo ni swali JE KIVULI CHAO KITAISHI AU KITAKUFA KAMA WAO? (fasihi)

Wapo wazee wetu wengi ambao Mungu aliwapa umri mrefu wakapata nafasi kubwa madarakani lakini HISTORIA IMEFUTA KILA KITU KUHUSU WAO yaani hatuna lolote jema la kujifunza kuhusu wao.

Hawa ni Watu waliomaliza Umri wao wote kuhakikisha WANAMFIKISHA FULANI KATIKA NDOTO ZAKE huku ndoto zao zikiteketea kwa moto mkali unaokula umri wao mfano mzuri katika taifa letu ni Mzee Mfaume KAWAWA.

Unaweza ukafanya mazuri mengi sana lakini mwishoni ukaumaliza umri wako kwa kufanya mambo ya hovyo mno au unaweza ukawa na mwanzo mbaya sana lakini mwishoni ukafanya mambo mazuri ambayo jamii na vizazi vyote vikakukumbuka. Mwisho mzuri hutengeneza historia nzuri.

Ukiwa mbinafsi ambaye malengo yake hayazidi urefu wa tumbo lake usitegemee kukumbukwa na yeyote labda funza watakalo kula mwili wako.

Tumia uhai na muda ulionao katika nafasi au kazi yoyote uliyonayo kuhakikisha kuwa umetengeneza kitu kizuri ambacho jamii na familia yako itabaki na jambo kubwa la kujifunza kwa mazuri.

Dunia ina watu wengi sana wenye akili na vipawa tofauti. Chagua watu sahihi wa kuwa karibu nao, usifuate mkumbo FIKIRI TOFAUTI, DAIMA UTAIBUKA MSHINDI

USIIGE MAISHA YA PUNDA MBEBA MIZIGO ASIYOIJUWA INA NINI NDANI
 
Mimi nitamkumbuka malaika mtukufu asiependa kukosolewa kwa ukabila makubwa na kwagawa watanzania ktk chuki kubwa
 
Back
Top Bottom