Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 42,334
- 56,542
Bwana yule alipingwa na kuandamwa hasa na daraja la juu(elites) la ndani na nje kwa pamoja kwa sababu hakuwa polished, alikuwa mtu blunt. Mawazo yake yawe mabaya au mazuri alikuwa akiyasema kwa namna ile ile tu bila kuremba, akikichukia alikuwa hajitahidi kuonyesha anakupenda, akikasirika au akiwa frustrated na jambo alikuwa anaonyesha wazi wazi hadharani, hakuwa mzuri kwenye mawasiliano ya umma, hakuzijua vizuri lugha zote mbili kuu muhimu za mawasiliano za watu wake. Alikuwa akionekana kama mshamba zaidi, tofauti na watoto wa mjini.
Jambo lingine la pili hakuwa na mawelewano mazuri na matajiri, alikuwa katika mapambano nao zaidi ,hakuwa rafiki wao wa kuaminika.
Ukiacha haya bwana yule hana tofauti sana na wengine. Waliyoyafanya au yanayofanyika hayana tofauti kubwa sana. Hakika historia itawahukumu vibaya wanaharakati uchwara na haitawasamehe kamwe.