Kwahiyo mbunge wako ni Mama Kilango.....Wapare wajanja sana lakini nawashanga mmeshamwoza huko Dodoma kwa Mzee Tingatinga lakini bado mnampatia ubunge.Samahani nimetoka nje ya mada kiduchu.
Mkuu mie naishi Dar miaka zaidi ya 30 sasa na huko Same ni asili yetu tu, sie tumetokea kijiji cha MESERANI WILAYA YA SAME
Mkuu Mtambuzi lakini mara chache si unakwenda kusalimia ndugu jamaa na marafiki au Shangazi,wajomba,mabinamu,mababu mabibi wadogo na wakubwa wote mmewasusa ?.
Mkuu nimeisha rekebisha pole sana mkuu!
pole sana shem Mtambuzi......
On a serious note...... tuna-share death day ya baba zetu (1/4), ila wangu ni 2007
RIP baba zetu......
tuliwapenda sana lakini tunaamini Mungu aliwapenda zaidi
ha ha haaaaaa, badala ya kuandika 4/1 nikaandika 1/4 lakini nilikuwa namaanisha January 4th, lol!Yeah nimeona shem, kuna tofauti ya mwaka mmoja.............
Katika jambo ambalo nilijifunza kwa baba yangu mpaka hata ndugu zangu wanajua ni kusoma magazeti na vitabu, baba yangu alikuwa ni mpenzi wa magazeti sana na hiyo tabia nimeirithi mimi peke yangu kati ya ndugu zangu wote, naamini ni kwa sababu nilikuwa karibu naye sana kuliko ndugu zangu, ila sasa mimi nimehamia mtandaoniiiiii........LOL
ha ha haaaaaa, badala ya kuandika 4/1 nikaandika 1/4 lakini nilikuwa namaanisha January 4th, lol!
hongera kwa kurithi tabia ya baba.....
mimi nilikuwa kipenzi cha baba lakini sina uhakika kama nimerithi chochote toka kwake.
ila ninachojua ni kuwa hapa nilipofika ni kwa sababu yake, nilikuwa namsikiliza sana kwa kila kitu ambacho alitaka nikifanye (isipokuwa kimoja tu)..... nilikuwa namwamini sana
ha haaaaaaaaa, mi sijui shem, lol!Kisaikolojia inaelezwa kwamba mabinti wengi huolewa na baba zao.
Namaanisha kwamba wale mabinti waliokuwa karibu sana na baba zao wanapofikisha umri wa kuchagua wenza, bila wao kujua huvutiwa na wanaume wenye sifa kama za baba zao, kama sio sifa inaweza kuwa sura, lakini itategemea zaidi kama binti huyo alikuwa anavutiwa na nini kwa baba yake. Haiyumkini ule msemo wa wanandoa kufanana pale wanapoishi pamoja kwa muda mrefu unaanzia hapo.
@FP, kama ulikuwa karibu na baba yako, basi hata mwenza wako ulimchagua/utamchagua kwa vigezo vya baba yako bila wewe kujua, huo ni mwito wa kimaumbile.
Nawaonea huruma wale mabinti ambao baba zao ni walevi kupindukia au wana mkono wa kupiga wake zao, nahisi ndoa zao hazitakuwa salama.............
ha haaaaaaaaa, mi sijui shem, lol!
ninachojua ni kwamba babangu alikuwa rafiki yangu so as mume wangu.....
Mkuu huyu RK ninani??....>>>>Pole sana mkuu mungu aendelee kuwapa nguvu na kuwa na mshikamano huo mliokuwa nao namwisho mungu aendelee kumuondolea adhabu ya umauti mpaka hapo siku ya kiyama!ili mkakutane tena kujenga familia moja!Amen