Tutajikumbusha hapa baada ya Makonda kushindwa vibaya kwa Mara ya 8

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,695
52,319
Kwanza nieleweke tu kuwa ningemuunga mkono Makonda kama tungewakamata wanaoingiza mizigo ya madawa Tanzania kutoka Pakistan,Brazil India,Colombia na kwingine kwa kutumia mgongo wa Wao kuwa wanachana wakubwa wa chama cha siasa kufika mpaka kuzima vifaa vya kupekulia mizigo Airport na bandalini ili tu waingize mzigo kuua ndugu zetu...

Wabunge maarufu,Mawaziri maarufu,Wafanyabishara wakubwa wameamua kuwaua vijana halafu leo unaenda kumkamata eti Chid Benz?......

Tupo serious kweli na hii vita ?

Makonda utashindwa vibaya sana vita Yako na madawa ya kulevya kwanza wewe mwenyewe anajua kabisa watu unaoshinda nao ni wakina nani na wametoka wapi wanafanya nini...............

Kwanza tayari ameshaanza kufanya makosa makubwa ya kisheria kitendo chake cha kumkamata na kumzuia mtu rumande kwa kumtuhumu kuwa anauza madawa ya kulevya bila kumkamata na mzigo kama alivyofanya kwa Wema Sepetu ni hatari na kesi inaweza kugeuka akipata wakili Mwenye weredi wa kumtetea ...........

Issue ya madawa ni issue sensitive sana huwezi kumtuhumu mtu bila kumkamata na mzigo wa Mali wenyewe eti kwa ushahidi wa kusikia tu kwenye udaku ndio maana kila siku mnashindwa kesi .............

Halafu eti unawatangaza police wanauza madawa na kesi yao unaipeleka police,police ndio washugulikie kesi ya police wenzao jamaa unachekesha kweli ulitakiwa wakati unatangaza kwenye vyombo vya habari files zao ziwe kwa DPP kwa ajiri ya kwenda Mahakamani na kufungwa moja Kwa moja............

Kufanya hivyo tu tayari umeshashindwa wala hakuna mjadala hapo........

Kumbuka hii ni vita ya kidunia usizani tycoon kule Pakistan, India,Mexico na Colombia watakubali kupoteza soko kwa sababu eti mkuu wa mkoa kakamata mateja Tanzania.........

Watu wa madawa kila nchi wapo kwenye system zote ndani ya mfumo na nje ya mfumo na uwa hawajibu kwa maneno wao ujubu kwa vitendo...........

Naomba huu Uzi uwe kumbukumbu kwa Makonda kushindwa tena kwa Mala ya nane ndani ya mwaka wake mmoja kama mkuu wa mkoa kama alivyoshindwa kwenye......

Makahaba......
Mashoga.........
Omba omba........
Wauza Shisha........
Watu kutolala Gesti mchana......
Nauli kwa walimu............
Kuandikisha watu wote wasio na kazi Dar...........
 
Technically nasubiria wale wabunge wawili,Millard nayo na Anayemiliki Redio na TV mawingu kama wataswekwa lupango au wanapewa dhamana au kesi.itafutwa kwa maana hakuna ushahidi.Jumatatu ni kesho kutwa tu.
 
Jamaa yangu haya uyasemayo yana ukweli ndani yake. Tena hii issue inaweza kummaliza mbwembwe zake zote. Anachokesea anaona hii issue kama vile anaweza kui handle peke yake kitu ambacho si kweli. Maana hii issue ni ya kidunia kama ulivyosema. Hivyo kuishughulikia kwake inabidi uwe mtulivu sana vinginevyo unapotezwa faster. Ni sawa na kupigana vita na mtu usiyemuona.
 
Kwa akili za bavicha ili uonekane msomi ni lazima usifie kila kinachofanywa na Saccos yao.
Yani wewe uwe ni kupinga kila kitu cha serikali alafu upongeze tu Mbowe hata kama anakwepa kodi!!!

Kama unawajua hao mapapa wa madawa hata wewe unaweza kuwataja
 
Mkuu ninaona kuna mantiki sana kwenye thread yako.

Kinacho nisikitisha ni namna viongozi wetu wanavyo fanyia kazi mambo ambayo ni sensitive na kuyafanya kuwa mepesi. Kwa ukubwa wa tatizo la madawa ya kulevya si suala la kuamka na kwenda kutangaza list kama ile ya akina chid benzi. Ninavyosoma majarida mbalimbali juu ya tatizo hili duniani hakika bado, kwa maoni yangu hii vita ni ya kuongozwa na Mh Magufuli mwenyewe akishirikisha vyombo vyake vyote siyo hii ya Makonda peke yake ila si mbaya kwa kuanza ili kubaini maeneo tata katika uwanja wa vita!
 
Technically nasubiria wale wabunge wawili,Millard nayo na Anayemiliki Redio na TV mawingu kama wataswekwa lupango au wanapewa dhamana au kesi.itafutwa kwa maana hakuna ushahidi.Jumatatu ni kesho kutwa tu.
Walitajwa hao?
 
Marekani kuna FBI na CIA ambayo ndiyo mashirika makubwa zaidi yanayoaminika kwa upepelezi wa hali ya juu duniani. Lakini bado nchi ya Mexico inaingiza madawa ya kulevya kiulaini mpaka sasa. Sembuse hapa kwetu Tanzania kirahisi namna kukomesha inshu ya madawa ya kulevya. Kwa upande wangu nasema ni jambo ambalo haliwezekaniki kabisa
 
Back
Top Bottom