Tutajifunza nini kutoka Zimbabwe?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,052
Reaction score
25,098
Kama mnakumbuka, Mugabe alitaifisha migodi yote na kuiuza kwa makampuni ambamo at least mmojawapo wa major shareholders ni mzimbabwe, halafu serikali inamiliki asilimia 40. Watu wa nje walipiga kelele sana na kudai kuwa hiyo ni seram mbaya ya madini, lakini naona inafanya kazi. halafu hapa Tanzania Kikwete anatuambia kuwa 3% tu ndiyo halai yetu na ni best deal pamoja na kuwa makamuni ya madini hayalipi kidi. Tutshangaa Zimbabwe iliyokuwa inadorola itakapoanza kutupa misaada. Nimesoma tena kuwa Air Zimbabwe inataka kuinunua Air Tanzania! Nadhani kuwa sasa wanaweza kuwa na uwezo huo!
 
pamoja na kelele zote zimbabwe tunaambiwa ni maskini lakini ina survive, asikudanganye mtu umaskini tunaoambiwa wanaowazimbabwe ni kwa vigezo vya wazungu vya GDP, si kweli hata kidogo, zimbabwe iko bettter off baaada ya kuwashugulikia wazungu kuliko walivyokua zamani na watarise sana! ni mfano wa kuigwa kwa nchi zote za dunia ya tatu, ila wenye kiherehere cha kukaribisha utandawazi kama sisi ndio tutalia sana uko baadae! we need mugabe of our own!
 
Siku zote ukitaka kuendelea lazima uchukue uamuzi mgumu..... kitu ambacho watanzania na hasa viongozi wa CCM na serikali yake wananogopa. Pamoja na yote hayo Air Zimbabwe ina ndege 7.....sijui ATCL ina ndege ngapi.
 
tunajifunza kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha nchi...
 
Siku zote ukitaka kuendelea lazima uchukue uamuzi mgumu..... kitu ambacho watanzania na hasa viongozi wa CCM na serikali yake wananogopa. Pamoja na yote hayo Air Zimbabwe ina ndege 7.....sijui ATCL ina ndege ngapi.

Inadaiwa ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…