Pole Anna Pita!. Pole sana kwa kuwa aliyekusaliti ni rafiki yako.
Je umeshawahi kujiuliza huyo rafiki yako alitumia mtego gani? Kila mtu anayo mapungufu yake, makubwa au madogo, hutegemea na mpimaji. Hata wewe unaweza, katika wakati wowte kuanguka mtegoni. Je unaamini kuanguka kwako katika zinaa inawezekana?
Amini nakwambia "Ikiwa kama wewe huna dhambi, na uwe wa kwanza kumpiga jiwe". Sis sote ni binadamu, kuna nyakati nyingi tunaanguka dhambini, ndio maana kuna fursa ya kutubu na kuungama.
Naomba ushukuru kwa kuwa umejua, hiyo itakusaidia kukaa na mchumba wako na kujadili kwa kina ili kujua udhaifu wake, kisha kumsaidia ili asitumbukie dhambini tena.
Nasema ushukuru kwa kuwa, kuna wanaume wasiri kana kwamba wanao vimada njia nzima, na mchumba wake hajui. Huja kujua baada ya ndoa, na mume kuichoka ndoa. Hivyo ndoa kuvunjika.
Mtu makini, akisha fahamu ufa, hufanya jitihada za kuziba. Kwa bahati mbaya sana, vijana wengi hutarajia kuwa na mahusiano yasiyo na kasoro. Hii haiwezekani. Haijawahi kutokea, tangu kuukmbwa kwa ulimwengu. Kumbuka uchumba wa Maria na Yosefu.
Fanya tathmini ya kina, juu ya kilichomwangusha mchumba wako, jitahidi kuziba ufa.
Najua wengi watakuambia umwache, jiluze, je kadiri ya tathmini yako, ni sahihi kumwacha??
Akili za kupewa changanya na zako.