Tutaiangusha CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaiangusha CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Sep 13, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Watu wengi tunaipenda CHADEMA na tunaombea ishinde uchaguzi ujao, lakini mimi natabiri sisi (Watz) ndio pia tutakaoiangusha CHADEMA iwapo itafanikiwa kuingia madarakani, na sababu ni tabia na mazoea yetu sisi Watz (waliowengi) ya kulialia na siku zote kupenda kumlaumu mtu mwingine hata pale makosa yanapokuwa yetu sisi wenyewe!

  Hivyo basi naamini huo mzimu pia utawakumba CHADEMA kwani watakapokuwa madarakani baada tu ya mwaka vilio vitaanza tena, wavivu wataanza kulialia, na visingizio kibao kama hawatusaidii, mbona maisha yetu hayabadiliki, wageni wamejaa wanachukua kazi zetu, tuondoleeni malipo ya parking za magari, umeme hautoshi wakati bili ya umeme hatutaki kulipa sasa sijui umeme unajizalisha, barabara za mitaani kwetu mbaya Mwenyekiti wa Serikali za mitaa akituita kwenye Mikutano kujadili matatizo ya mitaa yetu hatuonekani, Shule hazina madawati tukiitwa shuleni kwenye mikutano ya wazazi kujadili matatizo tuna mambo mengine muhimu ya kufanya kama kuangalia ManU na Chelsea, Maji hayatoki au hayatoshi huyo anayelia maji hamna ukiangalia anadaiwa na DAWASCO kwa miezi zaidi ya sita na kaunga maji ya kuiba!


  Hivyo nawashauri CHADEMA pia waanze kujiandaa kutukabili sisi Watz na kulialia kwetu
   
Loading...