Tutafakari neno 'Kalale mahali pema' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutafakari neno 'Kalale mahali pema'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzito Kabwela, Aug 7, 2011.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  Nimeona mahali pengi watu wakiitumia neno hili pindi mpendwa wao akifariki dunia. Wakristo wa madhehebu ya kikatoliki pamoja na waislam hutumia zaidi neno hili. Kufupisha wingi wa maneno tumeamua kusema RIP.
  Binafsi sioni umuhimu wa kumwambia marehemu maneno hayo kwa sababu zifuatazo
  1. Hakusikii/haelewi anachoambiwa maana roho imeachana na mwili
  2. Hajajitoa uhai yeye mwenyewe. Yupo aliyemtoa uhai na wote tunaamini kuwa aliyemuumba ndie anayechukua roho pindi mtu anapofariki. Huyo anajua hiyo roho ilale kwa amani au iale kwa vurugu.
  3. Sitaki niingie kwenye mambo ya kiimani lakini inaeleweka wazi kuwa kila nafsi itaonja mauti na baada ya kifo ni hukumu. Hukumu itafuatana na matendo ya mwanadamu awapo hai. Huwezi kuwa mzinzi, malaya, fisadi, tapeli, mwongo, mchawi na mtenda maovu mengine halafu ufe utegemee babako atamwambia Mungu akuweke mahali pema nawe utaenda huko. Hata logic ya kawaida sana inakataa.
  Ninachotaka tuelewane hapa ni kuwa Mungu anajua amweke wapi mtu wake anapokufa. Na sisi tunapaswa tuomboleze na kumshukuru Mungu kwa yote. Tusimfundishe/tusimwamuru Mungu amweke mtu mahala fulani wakati yeye mwenyewe ndo anajua pa kumweka.
  Changamoto tuliyonayo sisi tulio hai ni kutenda mema. Kama kweli tunaamini kuna mahali pema yatupasa tutende yaliyo mema ili tukifa hakuna haja ya matarumbeta wala mapambio wala kaswida(sijui jina halisi, mtanisamehe) ya kukumkumbusha Mungu pa kutuweka, mwenyewe atatuweka peponi
   
Loading...