Tutafakari maajabu haya katika ndoa

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,479
Reaction score
40,120
Wengi wetu tumekulia katika nyumba ambazo wazazi wote wawili walidumu katika mahusiano ya ndoa daima dumu. Ingawa kulikuwepo na vijistereotype behaviors kati ya mmoja wa wazazi hasa upande wa baba kuwa na mwelekeo wa mahusiano nje ya mama zetu. Lakini ndoa zilidumu daima.Tumeshuhudia mara nyingine kama si mara nyingi mama zetu wakiwa inferior mbele za baba zetu lakini ndoa zilidumu,Familia nyingi ziilikuwa na steps sons and daughters lacuna nod zilidumu

Mara nyingi kama si zote ndugu wa upande wa baba walijitahidi kutawala nyumba za wazazi wetu hasa kumkandamiza mama zetu lakini ndoa zilidumu.Nyingi za harusi za wazazi wetu hazikuwa za mbwembwe na classic kama zilivyo leo, ndoa zilifungwa kanisani kisha watu walitembea kwa miguu kurudi home huku kukiandaliwa ubeche (punje) nyumbani na kumbi zilikuwa ni makuti yaliyozungushiwa uani na kila mtu alialikwa kusheherekea muunganiko huo.

Maajabu ya leo ni kuwa mambo yamebadilika, Wakati wazazi wetu walichangiwa pesa na zawadi za kuanza maisha, sisi tunachangiwa mamilion ya kuteketeza one eve night ya reception. Kipindi hiki michango ya harusi imekuwa ni balaa, tunachangishwa mihela ambayo matumizi yake in a day ni tofauti kabisa na fedha ichangwayo. Sherehe karibuni zote zinafanyikia ukumbini na si nyumbani tena, waalikwa ni maalum tena ulinzi ni mkali.

Kumekuwa na figisu figisu kwenye tasnia ya ndo yenyewe. Kwani inaonekana kadiri harusi inavyokuwa na gharama na mbwembwe nyingi ndivyo inavyokuwa determined kukaa kwa muda mfupi kwani wanandoa wa siku hizi kuachana na kutalikiana ni kama ilivyo rahisi kuhamisha mtoto shule.

Nini kimejiri? Nini kinasababisha wanandoa wasisikilizane ama kuheshimiana ndani ya ndoa? Nini kimesababisha usaliti kufikia kiwango cha juu katika ndoa za leo kuliko zamani? Siku hizi mtu aliye ndani ya ndoa anaweza kuokota kabinti akakasomesha hadi kufikia viwango vya juu huku akikamiliki kama mke wake na akampangishia nyumba/ chumba bila wasiwasi. Siku hizi akina mama ndo wanaongoza kuchomoza na viserengeti boyz tena kwa fashion wanatambiana mitaani.

Nini kimepungua wakuu?

Kuna link gani imekosekana hapo kati hadi kufikia taasisi ya ndoa kuparanganyika siku hizi?

Tusake majibu, tuokoe ndoa zetu
 
Teh teh..Nafikiri kuwe na curriculum..some people need to cover some syllabus kabla hawajaingia kwenye ndoa..kuna wana ndoa humu uwa wanauliza maswali ya kitoto sana juu ya ndoa zao..Unajiuliza huyu ni mke/mume kweli
 
Teh teh..Nafikiri kuwe na curriculum..some people need to cover some syllabus kabla hawajaingia kwenye ndoa..kuna wana ndoa humu uwa wanauliza maswali ya kitoto sana juu ya ndoa zao..Unajiuliza huyu ni mke/mume kweli
Ni kweli
Wengi waliomo ktk ndoa kasoro hii imewakumba sana...
 
pamoja na harusi kuwa gharama bado ina umuhimu sana na zitaendelea kufungwa hamna namna
 
Times have changed. Back in the day, we old folks were groomed for the institution from a young age. Our women were taught to compromise for us, no matter what, and we knew how to respect them.

Nowadays, you young generation compete for everything. If he comes late, she feels like why shouldn't she? If he goes out with friends, she feels like she should do the same. Basically, no one's in charge. A team can't operate well with 2 quarter-backs all on the ground at the same time.

It's all about positions, and responsibilities.
 
Bila kugombana yanakua hayana stimu

Ruhusa kushikana lakini sio kushikiana simu

Fareed
 
Last edited by a moderator:
Tengeneza kwa audio... maana kiukwelii mTz ukitaka kummaliza ni kusoma prflect refuu hivyo na si mtihani ninao....
 
Bonge la research ila halina faida.
Haya maisha hayawezi kubadilika hata kidogo.
 
Mafunzo Na Mapokeo Ndy Yanayoleta Matokeo Kwenye Jambo lolote lile

Mkuu pamoja na hayo uliyosema lakin hata leo hii ndoa zenye furaha na Amani zipo ... Kwa nn zipo sabb wanandoa walifunzwa wakaelewa na wakaamua kuishi kwenye misingi sahihi ya ndoa

Kwa wale ambao hawakufanikiwa kupata mafunzo ya ndoa na wakahimili changamoto za ndoani maana yale ni kuwa Mungu aliwapa karama ya Hekima Busara Uvumilivu kuongozwa vyema ndoani


Kinyume na hapo ni matokeo ya unachokieleza mtoa mada (kutokuwepo kwa maadili ya ndoa )
 
utakuta ule muda wa kufunga ndoa na kulishana viapo wanaohudhuria ni watu wachache sana (wapambe,ndugu na marafiki kidogo) huku idadi kubwa ya watu wakisubiri tu muda wa kwenda ukumbini kwenye sherehe. unajiuliza kwani tukio lenye uzito ni kufunga ndoa au ni sherehe?
 
Bonge la research ila halina faida.
Haya maisha hayawezi kubadilika hata kidogo.
Mkuu ni wazi haupo kwenye mahusiano ya ndoa hivyo mada hii haina faida kwako. Tafuta partner mfikie kwenye viapo vya ndoa ndipo utaelewa namaanisha nini
Tengeneza kwa audio... maana kiukwelii mTz ukitaka kummaliza ni kusoma prflect refuu hivyo na si mtihani ninao....
BAdilika, badilisha mwenendo wako utaiokoa ndoa yako. Uvivu wa kusoma huletwa na vitu vingi vikiwemo KUPUUZIA.
LAkini unaweza ukakaa kwenye starehe kujirusha for hrs huku mkiongea pumba za maisha na mahusiano lakini kusoma vitu vya maana huna muda nao

Nakubaliana nawe kuwa hadi leo zipo ndoa za mfano wa kuigwa ndiyo maana ktk uzi wangu nilisema nyingi na sikumaanisha zote....
Ila kuna wimbi sasa la kupinga mila za kimapokeo hasa zinazohusiana na mahusiano ya mume na mke kwenye ndoa. Bahati mbaya jamii imegoma kuchuja aina ya mila za kuachana nazo na za kudumisha.
Tatizo lingine ni kuwa wazazi wengi hawana muda tena wa kukaa na familia zao hasa vijana wao ili kuwakuza ktk maadili mazuri bali watoto wameachiwa wasaidizi wa majumbani ambao nao ni watoto wanaohitaji maongozi, na waalimu ambao wapo full stressed na vipigo vya maisha pamoja na watumishi wa Mungu ambao wengi ni wa mshahara na si wito

Na baada ya sherehe bwana na bibi harusi wanakwenda fungate huku wakiwa na zigo la madeni......
 
Teh teh..Nafikiri kuwe na curriculum..some people need to cover some syllabus kabla hawajaingia kwenye ndoa..kuna wana ndoa humu uwa wanauliza maswali ya kitoto sana juu ya ndoa zao..Unajiuliza huyu ni mke/mume kweli

Upo sahihi sana mkuu na hili linakera sana kweli.
 

Words!!!
 
Tengeneza kwa audio... maana kiukwelii mTz ukitaka kummaliza ni kusoma prflect refuu hivyo na si mtihani ninao....

Huu ndio utoto unaozungumziwa humu ndani, watu wanaongea vitu vya maana unaleta masihala hapa.
 
Mkuu kikubwa MALEZI!! Mama zetu walivyolelewa na kizazi hiki kinavyolelewa ni tofauti.
Na kinachoharibu vijana wa siku hizi ni utandawazi. Kusema ukweli utandawazi kwetu unatanda vibaya. Tunatamani mambo makubwa yanayofanyika nchi zilizoendelea na sisi uwezo hatuna.
Utandawazi unahitaji knowledge ya kupambanua mambo na sio kuyapokea tu.
Sio kila anachofanya beyonce na wewe ufanye, au kila anachofanya Ronaldo basi nawe uige.
Hayo yanayoua vizazi vyetu kimaadili.

1.Malezi
2.Ukosefu wa Knowledge
3.Utandawazi.
Ningeshauri tuanze na hayo kwanza.
 
Malezi yamepungua na khofu ya mungu ....
 
Tatizo kubwa umelielezea hapo juu ukiwa unamjibu chalii wa ara...MUDA...jamii haina muda na kizazi kijacho. Fast life imetukosesha mengi.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…