Peterking1
New Member
- Jul 27, 2022
- 3
- 1
KIZUNGUMKUTI: Waweza ita hivyo ama vinginevyo, lakini katika hili linanipa shida kwa ninavyoendelea kukua, kuishi na kuyaona mambo yanayofanyika katika nchi hii. Najaribu kujiuliza ni lini basi mambo haya yatafika ukomo? Kila tunapoamka yapo na yanaendelea. Najiuliza ni nani basi ataweza kuwa suluhisho la mambo haya? Ama ni lini tutafika tamati katika kuchezea pesa za walipa kodi?
Ni siku ya jana tu, pale nilipopitia kwenye vyombo vya habari vya luninga, redio na mitandao ya kijamii. Ikawa na taarifa endelevu ya matendo ya ubadhirifu wa fedha katika miradi ya serikali. Siku ya jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipoamuru milango iliyowekwa kwenye moja ya jengo la hospitali ya Wilaya ya Namtumbo iweze kuondolewa na kuwekwa milango yenye hadhi ya kuendana na kodi za wananchi.
Si jambo jipya sana kusikia WM akitoa amri ya namna hiyo pindi anapotembelea miradi ya serikali. Hapa ndipo penye shida ya moyo wangu, hapa ndipo ninapokosa majibu. Kwa nini mpaka WM aje ndio mambo haya yaonekane yana shida?
Hivi hii miradi haina msimamizi kuanzia ngazi ya kata mpk taifa? Hivi hakuna mtendaji? hakuna diwani? hakuna mbunge? hakuna katibu tarafa wa wilaya/mkoa? Hakuna mkurugenzi? Hakuna mkuu wa wilaya? Hakuna mkuu wa mkoa? Vipi kuhusu kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na mkoa iliyojaa wataalamu, wachunguzi, wapelelezi, waendesha mashataka, wanasheria, polisi, magereza, jeshi n.k.
Hivi hawa wote haoni pindi haya mambo yanapotokea? Au ndio hayawahusu? Au wanakula pamoja? Kama hali ndio hii basi tutaendelea kuumia katika hali hiyo. Kwa kifupi inaonekana ni kama hakuna suluhisho la kutufikisha kwenye ukomo kwenye jambo hili.
Kwa leo tuishie hapa, tunapoendelea kujiuliza, huenda siku moja tutapata jibu la kututoa katika hali hii inayoumiza na kukatisha tamaa.
NI MIMI MTOTO WA MOROGORO
+255 682 527 228