The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Na: Sauti ya Mdodomia
20/08/2020
Dodoma.
Ukiachilia kelele mbalimbali ambazo watanzania wamekuwa wakizisikia kutoka kwa vikundi vya watu wachache nchini. Lakini watanzania watamchagua yule wamtakaye kwa manufaa yao na manufaa ya Taifa lao la Tanzania.
Watanzania baada ya kusikiliza kwa makini ilani ya CCM 2015/2020 na ahadi za Dkt. John Pombe Magufuli, walimchagua Dkt. Magufuli ili akayatekeleze yale ambayo ameyaahidi na yale ambayo CCM imemtuma akayatekeleze kwa ajili ya ustawi wa maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla.
Katika mambo aliyotumwa kuyatekeleza na CCM pamoja na yake aliyoyaahidi kwa miaka mitano inayoelekea kutimia siku chache zijazo, mhe. Rais Dkt. John P. Magufuli amekwisha yatekeleza na watanzania wameona. Watanzania wameshuhudia mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, ikiwa ni; kuboreshwa na kujengwa kwa miundombinu bora na ya kisasa, kuimarika kwa huduma za kijamii, ulinzi katika madini na udhibiti imara wa rasilimali za Taifa, pamoja na utunzaji wa mazingira kwa lengo la kuipa uhai ardhi na utawala bora.
Na kwa kuwa juhudi zake zilikuwa na msukumo mkubwa wa mapenzi ya dhati kwa watanzania na Taifa. Ni dhahiri shahiri kuwa IMF haikufanya makosa katika kuhakikisha ukweli huo unadhihirika kimataifa, mwaka 2019 shirika hilo la kimataifa la IMF iliutangazia Dunia kuwa Tanzania ni moja ya nchi baina ya nchi 10 za Afrika ambazo zinauchumi mkubwa. Ndio, ni nchi yenye UCHUMI MKUBWA! Afrika ni Bara ambalo sifa yake kubwa ni kuwa na nchi nyingi masikini, ambazo viongozi wake na watu wachache ambao wamejishika na viongozi hao ndio matajiri. Watanzania wameshuhudia kuwa kumbe Tanzania ni tajiri katika Afrika, haikuwa kazi nyepesi lakini Mhe. Rais Dkt. Magufuli ameifanya hiyo kazi ya kuinua uchumi wa nchi hata kufika kuwa ni moja ya nchi 10 Afrika ambazo ni tajiri!
Watanzania wanafahamu kuwa siasa za Dunia kwa karne ya sasa ni uchumi. Na kwamba hakuna uchumi, maana yake hakuna siasa. Leo hii Tanzania imeweza kutekeleza vema ahadi ya Ilani ya CCM kwa kuwa Rais Magufuli ameufanya uchumi wa nchi kuwa wa uhakika. Leo watanzania wanashuhudia Taifa linavyotekeleza miradi mikubwa ya maendeleo yenye thamani ya zaidi Trilioni 6! Wanashuhudia jinsi ambavyo huduma za elimu, afya na Maji ilivyokuwa ya uhakika kwa watanzania, wanashuhudia fursa za kiuchumi kwao kupitia miradi hiyo mikubwa.... Watanzania wameona na ni hakika yangu kuwa, wanataraji kuona mambo makubwa zaidi kwa miaka mitano mengine ya utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya jemedari Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa hiyo wataenda kumchagua Rais Dkt. Magufuli na CCM 28/10/2020...
Lakini kama ilivyokawaida palipo na mazao, magugu hayawezi kukosekana. Na kwa kweli hakuna namna ambayo utaweza kuyazuia ili yasijitokeze magugu hayo. Lakini watakaoenda kuvuna mavuno hayo watayajua mavuno ni yapi na magugu ni yapi, siku hiyo ikifika kwenye sanduku la kura, watachagua sahihi na magugu wataachana nayo. Magugu yanasema kwamba, jambo la muhimu ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu. Sasa, sisi CCM tunasema hakuna maendeleo ya watu kwanza kabla ya maendeleo ya vitu. Ndio ukweli huo, huwezi kutaka maendeleo ya nchi bila kwanza kupata mamlaka ya kujitawala, na huwezi kuleta maendeleo ya watu bila kwanza kuleta maendeleo katika vitega uchumi vya nchi. Na ndio maana kwa sababu hiyo, serikali ya CCM imeonelea haja ya kuanza kwanza na kuweka mazingira ambayo yatamsaidia mtanzania katika kukuza uchumi wake. Mtu hawezi kusema ameendelea akiwa hana uhakika na afya yake, hana uhakika na usalama wake, hana uhakika na uhakika na huduma ya maji na elimu, akiwa hana uhakika na upatikanaji wa nishati, hana uhakika na thamani ya mazao yake akiwa bado anayalima, akiwa hana uhakika na huduma ya nishati umeme, akiwa hana uhakika na usalama wa bidhaa zake wakati wa usafirishaji kutoka na ubovu wa njia za uchukuzi na usafirishaji n.k.
Kwa hiyo, ni watanzania wengi ambao wanaona haya. Na kwa kuwa wanaoufahamu mzuri kabisa, basi wanaiona ile dhana ya ilani ya CCM na nia njema ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuweka kwa pamoja maendeleo ya uchumi wa nchi na Maendeleo ya watu. Na ifahamike hata maendeleo ya watu yanayoonekana sasa katika nchi za ulaya yalitokana na Mapinduzi ya viwanda katika karne ya 18, ambapo kupitia Mapinduzi hayo nchi zilikuza uchumi wake na kisha kukuza uchumi wa watu wake.
Ndio kusema kuwa CCM ni chama chenye mikakati, sera na mipango yenye kuwezekanika kutekelezeka kwa kuendana na mabadiliko ya uchumi wa Dunia. Sera zake zipo wazi na utekelezaji wake upo wazi, na zinaenda kutoa majibu ya changamoto na shida za watanzania na zinaenda kuweka Tanzania katika nchi ambazo uchumi wake pamoja na watu wake ni wenye kuridhisha. Ni lazima watanzania wanufaike na rasilimali za Tanzania, na hatuwezi kuruhusu rasimali za nchi zipigwe na watu wachache na kisha watanzania kubaki wakinyonywa na wasifaidike na rasilimali zao.
WATANZANIA WANAZO SABABU MADHUBUTI ZA KUICHAGUA CCM 10/2020... NA WANAZO SABABU KAMILI ZA KUMCHAGUA RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI. HAWANA MPANGO NA MAGUGU!!!
Karibu Dodoma