Tusker Beer Vipi?

Tusker Beer Vipi?

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Posts
4,057
Reaction score
2,637
Jamani kwa wale tulioko Bongo, hasa tunaotumia ulabu aina ya Tusker tunateseka sas hivi maana Tusker zimeadimika kwenye mastarehe yetu. kuna anayejua nini kimetokea?
 
haijafa ila jamaa wa TBL wameamua kuacha kusambaza tusker kwa magari yao .wanaproduce na kuacha nje ili jamaa wa tusker wazifate na kusambaza wenyewe.kuna kajiuzembe kamefanywa na watu wenyewe wa tusker ndo maana ni adimu
 
ukweli ni kwamba TBL and EABL (watengenezaji wa Tusker) wamevunja mikataba yao na Serengeti breweries ndiyo itakayochukua jukumu la kutengeneza Tusker. Bado Serengeti hawajaanza hii shughuli na ndo maana kuna kiu mtaani.
 
TUSKER.. My Country My Beer.. kiu jamani
 
Tusker hamna lolote - Kunywa Serengeti Lager bwana!

Kila mtu ana kinywaji chake anachopenda, ndiyo maana kuna aina nyingi ili sisi tuchague. sasa sisi tunaopenda Tusker tunateseka sasa hivi. kwa wanywaji wa Tusker they know what I mean. Nimejaribu Ndovu, ladha yake imenishinda. I need Tusker
 
Jamani kwa wale tulioko Bongo, hasa tunaotumia ulabu aina ya Tusker tunateseka sas hivi maana Tusker zimeadimika kwenye mastarehe yetu. kuna anayejua nini kimetokea?
Hii tunaweza tukaita ni kinga ya biashara kwa TBL. Hawa EABL walipofunga virago baada ya ushindani mkali na promotion zenye rafu nyingi wakiwa wanatamba na bia yao ya kibo gold na promosheni ya jishindie gari. TBL waliamua kuichukua bia hii kwa mkataba wa kibiashara na eabl kwa kuwa ilikuwa inahitajika sana sokoni na bado ilikuwa na wateja wengi tu. TBL waliendelea kuizalisha hii bia, tatizo ni kwamba iliendelea kufanya vuzuri mno sokoni na hii maana yake ni kama TBL waliendelea kuipromoti bia ya wapinzani wao kibiashara na walikuwa wanawalipa kwa kila mauzo yanayofanyika kwa kutumia brand hii.

Ndipo hapo TBL waliona kwamba hii ni biashara kichaa na wakaamua kuiboresha Ndovu tuijuayo sasa chupa ndogo wakiamini itakidhi haja ya soko la tusker.
 
Shukrani kwa maelezo yako, Na je itaendelea kuzalishwa au ndo basi tena? Ingependeza zaidi kama hiyo Ndovu ingetengenezwa kwa formular ya Tusker, hivi tunashindwa kuiga kama Wahindi (Yaani copy and paste)?
 
Tusker itakuwa inatengenezwa na Serengeti Brewery very, very soon. TBL hawatengenezi tena Tusker, mkataba wao umekwishaaaaaa..

Ndiyo maana TBL wakatoa NDOVU ili watanzania muizoee mapema, wanywa Tusker subirini kidogo inakuja kutoka kampuni ya Serengeti, that is very good maana ushindani utakuwa mkubwa na bia zitakuwa na viwango zaidi.
Pia Serengeti wanajenga kiwanda kikubwaaaaa huko Moshi sijui wataleta brandy gani nyingine, tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom