Tusiwe wepesi wa kuhukumu

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,423
Kijana mwenye umri wa miaka 24 akiwa ndani ya treni alitazama nje na kupiga kelele...

"Baba, tazama miti inarudi nyuma!" Baba alitabasamu.

Watu wawili waliokuwa wamekaa pembeni walimtazama kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 mwenye tabia za kitoto kwa huruma huku wakimsikitikia.

Ghafla kijana alipaza sauti tena... "Baba, tazama mawingu yanatufuata!"

Watu waliokaa pembeni walishindwa kujizuia, wakamwambia yule baba..."Kwanini usimpeleke kijana wako kwa daktari mzuri amtibu?"

Yule baba alitabasamu na kuwajibu..."Nimeshafanya hivyo na ndio kwanza tumetoka hospitali, kijana wangu alizaliwa kipofu, leo ndiyo ameweza kuona kwa mara ya kwanza..."

Kila mtu hapa duniani ana stori yake. Usihukumu watu kabla hujawafahamu vizuri. Ukweli unaweza kukushangaza...fikiria kabla ya kusema kitu...!
 
Hivi kumbe eeh. Hata Judgement alisema Mamndenyi amechanganyikiwa kurudi ccm bila kujua kilichonivuta kwenda ccm.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Unakumbuka miaka ile ya bidhaa adimu?
Ukitaka sukari wanakuambia ni super market
na wakati mwingine ni lazima uzunguke mbuyu
ndo upate.

Unanipa kitu gani "adimu" kwa gharama ya utunzaji ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…