Tusiwavuruge Viongozi wa juu wa CHADEMA kwenye maamuzi Muhimu kuhusu Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiwavuruge Viongozi wa juu wa CHADEMA kwenye maamuzi Muhimu kuhusu Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Imnyagi, Jan 21, 2012.

 1. I

  Imnyagi Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya sifa kubwa ya chama chochcote makini cha siasa ni uwezo wake katika kufanya maamuzi sahihi kama ambavyo chama hiki kimekuwa kikifanya kwa nyakati zote.

  Kumekuwa na suala la kifo cha mbunge ambaye haijalishi alishindaje inagawa kuna tetesi nyingi kwa vijana wa Arumeru ambao walipigia CDM. Lakini Nasari hakushinda kama walivyotegemea kwa madai kuwa inaaminika kuwa kijana huyo aliuza timu kama ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa wenye tamaa ya Fedha na kukosa uadilifu na wengine walisema dogo aliitwa na wazee wakamwambia ampishe mkubwa ili akipata wizara fulani amkumbuke dogo katika ufalme wake na pia maendeleo yatakuja jimboni kama sumari atakuwa waziri na kama ataendelea kushindana na mkubwa huyo wao wana mbinu nyingi ya kuweza kulichukua jimbo hilo na hivyo ni bora akamate mshiko aendelee na masomo haya siyo maneno yangu ni ya baadhi ya vijana ambao ni wapiga kura wa jimbo hilo.

  Kuna mambo kadhaa nataka tuangalie kabla ya kumpitisha Nasari kwenye keybord bila kusubiri Busara na hekima za viongozi makini wa CDM. Kufanya maamuzi sahihi ya mtu atakayepeprusha bendera ya chama.

  CDM. Wanaandamwa na shutuma za ukabila, udini na ukanda kulingana na mawazo ya wasiopenda chma hiki hivyo tusitoe mwanya wowote wa kuwapa magamba upenyo wowote ule.

  Kumtea mtu kama Nasari ambaye alishakuwa mgombea ambaye kushindwa kwake kuna kasoro nyingi ikiwemo mwenzake alikuwa mgonjwa lakini bado akapita kuna hatari ya kulipoteza tena jimbo hilo.

  Kumteua Nasari wakati alishawahi kuwa mgombea tayari kutakuwa na madhaifu mengi ambayo ccm walishayaona na wakayatumia kumshinda hata sasa wanaweza kuyatumia na kumsambaratisha kabisa na CDM. Jimboni humo.

  Sina uhakika sana uwezo wake Binafsi yeye Nasari kama ni yeye tu ndiye mwenye mvuto na haiba ya kupeperusha Bendera ya CDM. Jimboni pale au aling'arishwa na chama chenyewe kama ilivyokuwa kwa madiwani waliofukuzwa. Hapa nazungumzia Quality ya mgombea na Quality ya chama pia.

  Ni vizuri kama tungeacha siasa za kishabiki makundi na ukabila katika kukishauri chama kuhusu mgombea bora kama kilivyofanya huko Igunga kikaleta matokeo mazuri kabisa na ule nauona kuwa ulikuwa ushindi.

  Viongozi wa Chama wapewe nafasi na suport kutoka kwa wanachama ili apatikane mgombea makini wa kuleta ushindi jimboni pale tuweke hisia zetu pembeni kwanza maana tunaweza kuwachanganya viongozi wetu wakatupatia Sauli badala Daudi halafu tukajuta baadaye hivyo tusiwavuruge viongozi wetu kwa hisia zetu kali na kuwachugulia mgombea kwenye keybord tuwape nafasi ya kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya chama na masilahi ya Taifa na siyo tuwashinikize kwa ushabiki zaidi pasipo kuchambua mambo kiundani.

  Zaidi sana tumalize kwanza msiba wa mzee Sumari itakuwa ni busara na adabu zaidi badala ya kuanza kupiga kampeni chafu za kichinichini tusiwe kama watoto ambao wanagombea urithi wakati baba hata hajazikwa bado.
  Nina imani kubwa na CDM.kwa uwezo wake na uzoefu wake kitatumia busara zaidi kuliko kufuata ushabiki,mashikinikizo na kampeni chafu za kichinichini.

  Mungu Ibariki CHADEMA.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 2. zululima

  zululima Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  a very strong point. umakini wa hali ya juu unahitajika. tuepuke mazoea. tuliona igunga. mgombea wa cuf alikuwa wa pili 2010 lakini miezi kumi baadae kwny by election hakuamini kujikuta akiwa wa tatu kwa kuambulia kura 2.000 tu. tufanye utafiti makini kabla ya kuteua mtu. kwa heri mzee sumari.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nyie Magamba huyu kijana Nassari anawanyima sana usingizi?
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CCM hangaikeni na mgombea wenu achaneni na chadema
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wewe CCM ufanye utafiti gani?
   
 6. I

  Imnyagi Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli ulio dhahiri kwamba CDM. Walifanya kazi nzuri sana Igunga na hii yote ilitokana na umakini wao katika kuamua mambo badala ya kufuata upepo wa watu wachache na matunda yake kwangu ulikuwa ni ushindi mnono wa moyoni kama alivyo Rais wa ndani ya mioyo ya wengi Dr. Willbrod Silaa.
   
 7. I

  Imnyagi Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nisengatamani sana kubishana na wewe kutokana na uwezo wako kuwa mdogo katika kuchambua mambo ki undani na kwa kutokuelewa au wewe kutumika vibaya tayari umeshampitisha Nasari kuwa mgombea kabla ya kamati kuu wewe nadhani hauna tofauti na madiwani walioasi ambao walifanya maamuzi yao bila kuwashirikisha kikamilifu viongozi wao juu na kuisaliti Damu ya wapenda mabadiliko kwa kuhongana vyeo.

  Unafanya kazi nzuri kwa huyo unayempigia Kampeni zisizo rasmi kabla ya wakati tena bila Idhini ya Kamati kuu na kamati kuu haiendeshwi kwa majungu na hisia kali kama zako ni kamati yenye Busara na inajua inachokifanya wakati wote kila mara ninaiamini na hata kama itamteua Nasari nitaona kuwa wao wameamua na wanachadema wote watampa ushirikiano lakini sisi humu siyo kamati kuu tunafanyia uteuzi kwenye keybord.
   
 8. V

  Vancomycin Senior Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huku ni kumpiga mtu vita haya maneno ya kusikia aliuza jimbo bila uthibitisho ni tatizo

  Joshua siku zote amekuwa mpambanaji katika siasa za Arusha
   
 9. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ushauri
  Nimekuwa nikipitia post nyingi sana humu na nimegundua kuwa mtu akitoa wazo tofauti na post zinazohusu chadema wengi wa magreat thinkers wanaponda sana! Mimi sidhani kama dhana hii ni nzuri maana inaondoa ladha halisi ya hili jukwaa! Kama kweli tunajiita magreat thinkers basi ni bora tuchangie posts bila kuonyesha mapenzi yetu ya chama. Kuna watu wana mawazo mazuri sana humu ila wanakatishwa tamaa na wapenzi wa chadema. Ni vema tukawa flexible ktk kuchangia mawazo bila kuwa na mtizamo wa kichama ama chochote kinachohusiana na hicho! Hili ni jukwaa la siasa hivo mawazo ya mtu yaheshimiwe kama alivyoyatoa ama positively or negatively! Ingawa wengi wetu tunaamini hii jf ni ya chadema kulingana na member wengi wanavyokuwa wakali pindi viongozi wao wanapoguswa humu,basi tuwe na kiasi ktk kuponda mawazo ya watu wengine. Naomba tuheshimiane sisi kwa sisi kama kweli tunataka kusonga mbele ktk kuijenga nchi yetu. Sisi sote ni wamoja!!!!!!!!!!
   
 10. I

  Imnyagi Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijawahi hata kuwa karibu na huyu Nasari ila nimemsikia kwenye mikutano na zaidi sana ninatoa kama ushauri kwa wenzangu kuhusu kuheshimu mamlaka ya kamati kuu katika kufanya maamuzi sahihi na siyo kumpiga vita Ya maneno Nasari na hata kama akiteuliwa yeye wanachadema wote watamuunga mkono lakini tuache kampeni chafu za kichinichini kwenye keybord halafu tukapoteza ushindi muhimu kwa jimbo muhimu.

  Kuhusu usaliti wa kuuza hayo ni maneno ya baadhi ya wapiga kura wake ambao mpaka leo hawaamini kuwa kwa kura walizoipigia CDM. Halafu ushindi uende ccm. Haina maana kwamba nimemuhukumu moja kwa moja ni tahadhari tu kama nilivyowahi kusema kuhusu Shitambala kule Mbeya na watu wengi walishambulia sana ila baada ya muda mfupi majibu yalijidhihirisha na kila mtu aliona hilo.
   
 11. I

  Imnyagi Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama una uhakika na unachokisema mimi ni Chadema Damu na ni haki yangu kutoa maoni yangu kwa ajili ya uhai na maendeleo ya chama chetu kwa siku za baadaye.
   
 12. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,143
  Likes Received: 1,711
  Trophy Points: 280
  matokeo ya 2010 Ubunge Arumeru Mashariki
  Sumari 34,661
  Nassari 19,123

  Kijana alijitahidi na ana mtaji tayari wa kuanzia , CDM imuendeleze tu na kumuongezea nguvu
  kama kweli ina nia ya kuwaedeleza vijana wenye uwezo na nia
  BTW , No offense ila kura za Dr Slaa Arumeru Mashariki hazina tofauti sana
  na za Nassari ,
  JK 32,257
  Dr Slaa 21,330

  kwa hiyo kumchagua Dr Slaa hakutakua na faida sana kwa CDM ,
  zaida ya CCM kutaka kumuangusha Dr Slaa kwa gharama yeyote ile
   
 13. I

  Imnyagi Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hapa ndipo tunapokosea na kuwazuia hata wengine wenye uzoefu na kujua baadhi ya mambo muhimu yanayohusu chama kwa kuwaogopa watu wachache walioko humu wenye jazba na tamaa ya madaraka na kupiga kampeni chafu badala ya kuishauri Kamati Kuu kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya chama.
   
 14. D

  Derimto JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ngoja waje wenye Chadema yao ambao hawapendi mawazo yoyote ya busara bali muda wote wanataka ubabe na kushaurika kwao ni vigumu.
   
 15. bona

  bona JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  wengi ambao si wakazi wa arusha tungependa kupata cv yake kwanza na background kidogo kilichotokea kwenye uchaguzi uliopita maana wengi wetu tulikua bize kufuatilia majimbo yrtu na kara za urais ila in short sidhan kama ni vizuri kumrudisha mgombea aliyeshindwa 'CLEANELY' kwenye uchaguzi uliopita unless kuawe na ushahidi kua either aliibiwa au kuna mchezo mchafu uliotokea!
   
 16. MZEE WA ROCK

  MZEE WA ROCK JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 623
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tumeanza mapema sana kampeni ktk jimbo hilo. tusubili hata matanga ya mzee sumari yaishe, tusiwe km watoto wanao taka uridhi wakati baba yao hata hajazikwa. tuwe na uvumilivu lidogo wana jamii wenzangu. tukianza hvyo kesho mtaleta nani ni mrithi harali wa dada REGIA.tuwe wastahimilivu kidogo ktk mambo muhimu, UUNGWANA NI VITENDO.
   
 17. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  yaani CCM mnapropaganda za kitoto sana na kijinga mno... mnamjua Nassari vizuri, kwanza niseme uchaguzi ulipoisha Nassari hakwenda kulala aliendelea kukesha kama mbunge wa jimbo lakini wawananchi kitendo hicho kilimfanya Nassari kuwa karibu na wapiga kura wake kwa muda wote bila kujali ni kipindi cha kampeni ama la, Nassari alikuwa akishirikishwa na viongozi mbalimbali bila kujali itikadi za dini zao na vyama vyao katika muendeleezo wa maendeleo ya jimbo hilo.

  Wananchi wajimbo hilo walimuona Nassari ndiyo kimbilio lao pale walipokuwa na shughuli za kijamii bila hiyana Nassari alishiriki na kufanikisha shughuli hizo kwa kiwango kikubwa sana kwa kushirikiana na rafiki zake wakaribu, shughuli hizo ni pamoja na harambee mbalimbali, upandaji wa miti, ujenzi wa madaraja nk. kwa hayo kila mtu avune alichopanda Nassari anafaa kwa ARUMERU na nitishio kubwa kwa ccm. usifananishe igunga na ARUMERU hata historia inakuhukumu.......... NEVER SAY NEVER
   
Loading...