Tusitupe Majina Ya Ukoo

Hata wasio na asili ya Afrika kama Richard Mabala

No Mabala hii thread si yake maana yeye katupa jina la ukoo wake, hii thread ni ya kutotupa majina ya ukoo/ asili ya mtu.
 
watoto wangu wote wana majina ya asili na la ubatizo... sitaacha kutumia majina ya asili!

bongo kuna sharlene, Sharon, alvin, beyonce, madeleine, etc... sasa sikiliza watoto wenzao wanavyoyatamka, ni kituko!!!

Ndipo hapo mtoto anaitwa Sean kama Diddy Combs, lakini mtaani wenzake wanambadili jina anakuwa "Shani".
 
Mh lakini kuna majina mengine ya ukoo kuyatamka tu inabidi uende tuition akaaa mie nabaki na hili hili langu la Sharleen Davis mpaka mwisho.

Lily Flower,
Kumbe jina lako Sharleen Davis, safi sana.
 

Mwanzisha mada amegonga panapotakikana. Ulimbukeni huu upo hapa hapa JF, achilia mbali huko shuleni na kna kazini. Angeanzia kurusha madongo hapa JF, maana hapa napo wamejaa wazungu kibao!
Utakuta kuna majina kama
Babylon
First Lady,
Lily Flower,
Invincible
Field Marshal
PlanckScale
n.k.

Kwa nini msitumie majina ya ubin kama Idimi, Mwanakijiji, Mkandala, Nyamayao. Nguli, Kiranga, Nzalalila, Mwakisu, Rwegoshora n.k
 
Sasa kuna wengine hawataki kabisaaaa kusikia wakiitwa majina yao ya utoo......... YALE YALE YA NYAGEMA ANATAKA AITWE 2PAC
 
Kweli kabisaaaaaaaa................ kitu NGALIKIHINJA bwana .....full kibantu
 
ni kweli mkuu!majina kama
MGOLOLA FINYONGE
CHAMVANGA
MWAKYUSA
KITUTILE
MBOMBO NGAFU
I FIINGI FI DSUMBAGE
CHANIKA
UU LUKALIKALI LWA NNJWAA
IDENYIMEMBE
MAKISHEKE
UTUDAHO

haya ndo majina yetu na mila zetu zitaendelea kudumu kama tutakuwa na majina haya
 
Thijakuelewa.........yaani unasapoti halafu jina lako LINAPINGA.........!!!!????
 
Thijakuelewa...............yaani mpaka utukonvisi ndo tuone kuwa username yako ni ya kibantu.......???!!! Inatakiwa liwe linajieleza lenyewe............yaaani mpaka ulikate ulimege na kulidismento ndo lionekane la kibantu............ hebu cheki kitu hili CHIMUNGURURU............ yaani chenyewe kinasema huna haja ya kusidismento wala kua-n'disimento
 
No Mabala hii thread si yake maana yeye katupa jina la ukoo wake, hii thread ni ya kutotupa majina ya ukoo/ asili ya mtu.

Nimekupata mkuu, lakini it is interesting kwamba huyu mzungu ka-adopt jina la Mabala solely because he wants to associate himself with his new "found land". Some of us are doing precisely the opposite - choosing names that are disassociating us from "our land".

I could have forgiven wabongo ambao wamehamia, let's say Ujerumani, nakuona umuhimu wa kuadopt to Germans names. Lakini si hivyo ndugu yangu. Unamkuta Myakyusa (au Mpare) anajiita Peter Lucas hapa hapa bongo...😕
 
tatizo la wa Africa (Tanzania), tumekubali kwa kiasi kikubwa kuwa brain washed kwa asilmia kubwa, unakuta mtoto anajina zuri tu la kiafrica lakini likitamkwa watu wanamcheka , lakini la kiingereza lenye maana sawa na hilo linaonekana ni bora

mfano- SMITH ni sawa kuliko MFUACHUMA
BELL ni sawa kuliko KENGELE
McNIGHT ni sawa kuliko CHAUSIKU
 

Watanzania wa bara wengi walikuwa wakitumia majina ya ukoo, nadhani siku hizi wamepunguza labda kwa sababu ya chimbuko la ukabila linalotishia sasa hivi. Lakini mikoa ya pwani watu wengi wanatumia majina ya baba zao sana kuliko kutumia majina ya ukoo. Kwa mfano nenda Lindi pale sokoni ukatamke Amina Ali, au Amina Saidi or my favorite Somoe Saidi. Watu mia tau hivi watatokea kwa jina moja. Itabidi useme unamtafuta Somoe gani ndipo qualifier itakapotolewa Somoe Saidi Nachenga or Somoe Saidi Mtumbatu etc.

Pia nimewahi kukutana na mke aliyekataa kuwapa watoto walke jina la ukoo la mume wake kwa sababu alisema linasound too kikabila cha huyo baba. ( needless to say it sounded funny and childish but they are her children)
 
duhh sasa nikuulize swali hawa watoto wa metro utawafanyaje. Kizazi kipya cha mchanganyiko wa makabila babu morogoro bibi mbeya baba morogoro (ndio kwetu huko) mama mozambique, baba dar es salaam lakini kwanza bibi na babu ni dar es salaam na kigoma duuh na ndugu zangu waluguru majina wanasola kwa wajomba zao ha ha ha ha we usiseme lakini hii inajadilika nikiumuita mwanang mwajabu mbona watu wanachemka, majina ya uswahilini. Nikienda kumwita mwanagu mwamba (tafsiri ya Petro) jamaa hawambatizi duhh na mimi mkristo he he he yaani hii inajadilika kwelikweli lakini tunahitaji watu wa saikolojia na sosholojia wanaoujua mbele na nyuma, mtandawazi na utandawazi na kisha homa ya majina ya wachezaji wa ligi ya kiingereza teh tehe na tena homa ya kizazi kipya majina yasiyotamkika peng peng duhh hii inajadilika halafu tamu kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…