Tusitishe ya Shonza...

Tusitishe ya Shonza...

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
WanaJF
Naona ni wakati sasa tuache kumjadili huyu mwanadada geugeu, asiye na msimamo, na mwenye kuyumbishwa na kusongwa na tamaaa sijui ya vyeo au ya fedha au...

Nasema hivi kwa sababu kwa takriban wiki tatu sasa amejitokeza katika sura nyingi tofauti: kuwa ameonewa Chadema- kwa kumfukuza, kuwa yeye ni mjumbe halali wa Bavicha, hatambui kufukuzwa, baadaye ajabu yupo CCM, akinyoosha ngumi, sasa eti ana mkakati wa kuhakikisha Mnyika anatoka Ubungo..... na sura nyingine nyingi ambazo tumeshuhudia kwa kipindi cha takriban wiki tatu. Daima tumeona yeye mwenyewe amekuja ama kukanusha kitu fulani, au kuja na utetesi fulani kupinga jambo fulani lililosemwa, ambalo kimsingi ndiyo ukweli wenyewe, unaokujadhihirika muda mfupi baada ya yeye kukanusha

Ni kwa sababu hii, naona wanaJF, tuache kujadili yanayomhusu: tujadili mambo ya msingi kuliko kujadili mambo ya mtu ambaye ameshaonesha udhaifu mkubwa katika yale anayotamani kuwa nayo; hawezi kuwa hata kiongozi wa nyumba kumi kwa maoni yangu, maana atawasaliti kwaajili ya ugeugeu wake.

Labda kwa vile yeye pia yupo humu, na kina Nape, Mwigulu na wengine wa chama chake kipya wajadili wanayoona yanafaa, labda wabuni mbinu mpya za kutufisadi watanzania, wasitupotezeee muda wetu adhimu...

MOD kama mtaona inafaa, nitafurahi zaidi hii post isipounganishwa na nyingine... ni ombi tu..
 
CCM pokea oil chafu @Nape why washangilia oili chafu au umesahau?
Shonza&mpamba msije kwenu Mbozi mmetia aibu tutawazomea wasaliti wa mageuzi. Sasa mpamba matusi uliyokuwa unayatoa kwa Zambi mb sura yako utaiweka wapi? pia utagombea ubunge jimbo lipi? RIP.
 
Mwampamba na shonza mnakufa kisiasa mapema mno. Because both of you are very young, hakika ccm itakutumieni kama condom kisha maisha yenu jalalani au chooni kwisha!
 
Tutasitishaje ilhali wewe umeanzisha uzi wa kumjadili!?? acha tuendelee kumpaisha
 
Ni kweli kwani inampatia umaarufu asio nao. Huyu dada ni mtu fake....mume atakyemuaoa achunge sana maana kutokuwa na msimamo kiaisi hiki kuweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa yake. inaonyesha ana-price tag usoni mwake
 
Back
Top Bottom