Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Wale wavuvi wa samaki wanafahamu chambo kinavyotumika kumnasa samaki. Si kitu cha kushangilia hata kidogo kwa rais Magufuli kuruhusu wimbo wa Ney wa Mitego ambao BASATA ilikuwa imeufungia.
Naiona ruhusa ya Magufuli kama chambo cha kunasia wananchi. Kuruhusu kwa namna alivyofanya Magufuli kunamjenga na kumwonyesha kama mtu mweye funguo za kufunga na kufungua chochote hapa Tanzania, kitu ambacho si kizuri hata kidogo.
Kwa rais kuwa na funguo ya kufunga na kufungua maana yake ni kwamba taasisi zote za umma na zingine zinakosa maana na wala hazitafanya kazi kwa kujiamini. Matokeo yake ni kwamba taasisi na wananchi wanajengwa na kuzoeshwa kisaikolojia kuwa maamuzi katika nchi hii yanafanywa na mtu mmoja, ambaye ni Magufuli. Tafsiri ya hali hii ni kukosekena kwa demokrasia na utawala wa sheria. Na inafahamika fika kuwa kama hakuna demokrasia wala utawala sheria, maana yake ni utawala wa kiimla (Dictatorship).
Kama Magufuli alikuwa na lengo la kujenga taasisi za umma na si kujijenga yeye binafsi ilitakiwa BASATA na jeshi la polisi ndio waseme kuwa wamechunguza kwa makini na kuona kuwa maudhui yaliyomo katika wimbo wa Ney yana ujumbe ambao una manufaa kwa taifa kuliko hasara. Kwamba wimbo huo kwa mtazamo mpana una mafunzo mazuri.
Tukizoea kuamuliwa kila kitu na rais, mwisho wa siku msemaji katika nchi hii atakuwa mtu mmoja, si taasisi za umma wala nini bali Magufuli. Na hapa ndiyo tatizo lilipo.