Tusisahau: Muhimili wa mahakama unajua kuwa Tundu Antipas Lisu ni mgonjwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,031
142,090
Ni katika kukumbushana tu kwani Tundu Lisu ana kesi pale mahakama ya kisutu.

Kuna wakati lilipelekwa ombi mahakamani kwamba dhamana ya Lisu ifutwe na mdhamini ajitoe kwa kuwa Lisu ameshindwa kuhudhuria mahakamani bila taarifa.

Hakimu alilikataa ombi hilo kwa kusema kuwa Tundu Antipas Lisu ni mgonjwa na taifa zima linajua.

Mwenye masikio na asikie
Maendeleo hayana vyama!
 
Aamen
 
Unajua shetani hakuridhika baada ya uamuzi huo wa hakimu ndio akapanga mbinu hii mpya ya kishamba na kilimbukeni .
 
..Spika anajua kuwa TL ni mgonjwa.

..ila ameamua tu kumfanyia ukatili.

..nadhani kosa la TL ni kuonyesha kuwa anapata nafuu na kuonekana ni mtu mwenye furaha na bashasha.

..tangu wamuone anakula mshikaki basi wameanza kumuandama utafikiri amekula nyama ya binadamu.
 
Office ya speaker haijawai kupata barua yoyote kutoka kwa lissu au kwa mwanasheria wake.Kingine ni kwamba katibu alileta urafiki kumuandikia barua kaka yake kutaka kumuuliza mdogo wake yuko wapi lakini lissu hakujibu,nadhani hana mawasiliano mazuri na kaka yake aliyemlea learned brother Alute Mwighai.
 
Akili yako inakusaidia tu kukwepa usigongwe na Bajaji. Meaning...uwezo wako wa kufikiri ni level ya sisimizi...
 
Kwani Lisu alijeruhiwa akiwa jimboni kwake au bungeni?!
 
Pasingekuwa na kifo binadamu wangeoneana sana......hivi tu kwamba kila nafsi itaonja mauti lakini kuna watu wanatenda kana kwamba wataishi milele!
 
Kama ni hivyo (kwamba Mahakama inajua Lissu ni mgonjwa) kelele zote za kumdhihaki Spika ni za nini? Lissu, ambaye ni mwanasheria, si aende tu mahakamani 'amkomoe' Spika amrudishie ubunge wake. Hapo ndipo tutajua mwenye busara ni nani. Haimsaidii cho chote Lissu kukaa akilalamika mitandaoni.
 
Kwani akilalamika mitandaoni anakuwa amekiuka kifungu gani cha katiba ya JMT?!!

Maendeleo hayana vyama.
 
Mungu ni Mkuu mno kuliko tunavyoweza kuwaza, kutoka kwenye kutaka kumwua Lissu akapona mengine yote yatapita tu endeleee umwandama ili siku akiinuliwa mshangae !!!
 

Yohana ahsante kwa kuona hilo...ila chama chako na genge lake la waovu hawapendi kumwona Lissu akiwa ana uhai...
 
Yohana ahsante kwa kuona hilo...ila chama chako na genge lake la waovu hawapendi kumwona Lissu akiwa ana uhai...
Tatizo Lisu naye anautaka Uenyekiti wa Chadema taifa kwa nguvu zote na Job na Freeman ni marafiki wakubwa.
Unakumbuka Job aliporejea kutoka India kwenye matibabu kamanda Aikael alishinda pale salasala siku nzima kumfariji mgonjwa!
 
Tatizo Lisu naye anautaka Uenyekiti wa Chadema taifa kwa nguvu zote na Job na Freeman ni marafiki wakubwa.
Unakumbuka Job aliporejea kutoka India kwenye matibabu kamanda Aikael alishinda pale salasala siku nzima kumfariji mgonjwa!

Hilo sasa ni ramli mkuu....kumfariji mgonjwa ni tendo jema tena ukilifanya kwa adui yako
 
Anaandika Askofu Dr.Benson Bagonza Askofu wa KKKT jimbo la Karagwe

Kuna tofauti kati ya BUNGE na BONGE.

Bunge huongozwa kwa mujibu wa Katiba Sheria Kanuni Tamaduni za mabunge mila na desturi nzuri busara na hekima.

Kikikosekana kimoja kati hayo juu,linageuka kuwa Bonge,maana yake BONGE linatisha linaonea linapendelea linahujumu linajihujumu linajichanganya linalipiza kisasi linakera BONGE halina utu wala huruma.

BUNGE letu sio BONGE,Mungu ibariki Tanzania
Libariki BUNGE letu liepushe na majaribio ya kuwa BONGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…