Tusipostuka tutaendelea kuwa ma-mbumbumbu

Tusipostuka tutaendelea kuwa ma-mbumbumbu

MaMals

Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
46
Reaction score
8
Baada ya kushindwa kusoma makala iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza; nimekaa na kutafakari. Pamoja na kupita madaraja kadhaa ya kielimu (mpaka chuo kikuu) lakini nimeshindwa kuambulia chochote katika makala ile. Nadhani maarifa yale yangenifaa mno. Pia nadhani kutoilewa lugha ya hii; ndio moja ya sababu Watanzania wengi wana IQ ndogo simply because wanashindwa kupata maarifa mengi ambayo yameandaliwa kwa lugha ya kigeni. Katika afrika mashariki nchi ya Tanzania haijachangamka kama nyingine mfano tukio la hivi karibuni la kutekwa kwa mabinti huko Naigeria wananchi wa Kenya wamekuwa wa mwanzo kulaani tukio hilo,

Tanzania wamestuka baadaee..simply because wenzetu wanafuatilia media za kimataifa kwa ukaribu na wanaona uzito wa masuala wakati Watanzania wengi tunasubiri vyombo vya habari vya ndani ambavyo mara nyingi havitoi uzito stahiki. Tanzania kuna tabaka kubwa sana; wajua English na wasiojuwa. Wajuaji ambao wengi ni wasomi (influential peoples) na ma-policy makers wanang'ang'ania lugha ya Kiswahili ati kwasababu ya utamaduni Sikatai lakini lugha ya kiingereza ni muhimu vile vile na inapaswa kupewa kipaumbele shule zetu kuanzia elimu ya msingi. Kuna nchi kama Zambia wameipa kipaumbele lugha ya kiingereza lakini bado lugha za ndani zinatumika vizuri tu.

Unafiki wa wajuaji ni kwamba; kwa sababu wanaijua vyema lugha na wanafyoza maarifa mengi ilhali bado wanatugeukia tusiojuwa wanatuambia tutumie lugha ya Kiswahili. Hali kadharika kwa sababu wao wanaijuwa umuhimu wa lugha ya kiingereza basi wanawapeleka watoto za katika shule za English medium, halafu watoto wa akina sie wanapitia katika mfumo mibovu ya kielimu, Wallahi huku ni kupunjana. Uandaliwe mfumo wa kusawazisha tabaka hili. Viongozi wetu walikosea sana kuipuuza lugha hii na bado tutaendelea kukosea kama hatubadili sera zetu.
 
Baada ya kushindwa kusoma makala iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza; nimekaa na kutafakari. Pamoja na kupita madaraja kadhaa ya kielimu (mpaka chuo kikuu) lakini nimeshindwa kuambulia chochote katika makala ile..

Makala gani hiyo mkuu nikusaidie kuitafsiri.
 
Back
Top Bottom