Tusipokuwa makini, Tozo zitazalisha EPA nyingine au ufisadi Mkubwa mwingine

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
17,286
10,667
Tunaimbiwa mapambio mazuri kila siku kwa sababu ya Tozo.

Tozo inajenga madarasa

Tozo inajenga vituo vya afya

Tozo sijui inajenga barabara

Tozo imeleta sijui vitu kedekede

Wakati huo huo tunakopa mabilioni na mabilioni kutoka taaisisi mbalimbali za fedha.

Sasa hayo madarasa yanajengwa na Tozo au mikopo?

Halafu hata hivyo ukizunguka kwenye mashule ya msingi na sekondari hatuoni ujenzi wowote ukiendelea, tulitegemea kila shule ya sekondari au msingi wangekuwa bize kujenga madarasa,lakini hatuoni kitu.

Hivi hatupigwi kekundu kweli kwenye TOZO?

Isije ikawa wenzetu wanaandaa hela za kampeni 2025 kwa mgongo wa Tozo?
 
tukizubaa watanzania hizi tozo ndiyo utakuwa utamaduni wa CCM kukusanya mapato kwa njia hii, hizi TOZO na ile kodi ya kichwa, baskeli na mifugo enzi za ukoloni zina tofauti gani. Tuamke tuseme tozo NO.

Kwa mfano mimi mfanyakazi nalimwa PAYEE 30% ya mshahara.
Nakwenda kununua kitu kutumia mshahara huo huo nakutana na VAT 18%
Nakwenda kutuma hela kwa wazazi ama ndugu nakutana na rungu la Tozo tuseme 4%

Hii si haki kabisa, yaani mshahara wangu tunaugawana nusu kwa nusu kwa mwezi 50% yote inaondoka - hapana aisee.
 
Dah hapa kwa watumishi wa umma aisee kitanzi kila ukigeuka umekula kibano...

Hizi tozo Hakika Ni bomu Sana ...
 
Hangaya nchi ishamshinda hii/// ndani ya chama chake wanamhujumu kupitia hii tozo
Tunaimbiwa mapambio mazuri Kila siku kwa Sababu ya Tozo.
Tozo inajenga madarasa,
Tozo inajenga vituo vya afya
Tozo sijui inajenga barabara,
Tozo imeleta sijui vitu kedekede.
Wakati huo huo tunakopa mabilioni na mabilioni kutoka taaisisi mbalimbali za fedha.
Sasa hayo madarasa yanajengwa na Tozo au mikopo?
Halafu hata hivyo ukizunguka kwenye mashule ya msingi na sekondari hatuoni ujenzi wowote ukiendelea,tulitegemea kila shule ya sekondari au msingi wangekuwa bize kujenga madarasa,lakini hatuoni kitu.
Hivi hatupigwi kekundu kweli kwenye TOZO?
Isije ikawa wenzetu wanaandaa hela za kampeni 2025 kwa mgongo wa Tozo?
 
Back
Top Bottom