Tusingempata Magufuli Taifa lilikuwa linazama na kupotea!

Long live Magufuli
Screenshot_2021-03-18_005052.jpg

ATAKE ASITAKE🐒🐖😂😂😂😂
 
Rais Magufuli amekuja kama mkombozi wa pili wa Taifa hili la Tanzania.

Hajaja kutengua torati bali kuielezea na kuitekeleza torati kwa lengo lile lile ambalo Mwenyezi Mungu alilipanga kwa nchi yetu.

Taifa letu lilifikia mahali patakatifu kwa wezi,mafisadi,matajiri wanyonyaji na wanaojali maslahi binafsi.

Taifa liliingia kwenye mfumo wa kibepari pasipo kujipanga na matokeo yake ni kuiga kila kitu cha mabepari bila mpangilio au lengo kama nchi.

Taifa lilikubali kuingia kwenye mfumo mpya wa unyonyaji unaofanania na utumwa au ukoloni wa enzi zile.

Tanzania yetu ilibakiza hatua chache sana kuruhusu ushoga,biashara za miili na mabaya ya namna hii ili kukidhi matakwa ya watawala wa kikoloni.

Baada ya Uhuru tulijitahidi kuweka mfumo wa uendeshaji wa nchi yetu lakini matakwa ya wakoloni yalituzidi nguvu na hatimaye tukaamua kuyakubali kama sehemu ya mfumo wetu...yaani tukaacha njia bora za kufuata na tulizojipangia kuzifuata kwa ustawi wa Taifa letu huru.

Wakati na punde baada ya uhuru tulijiwekea malengo na mikakati mizuri kwa ustawi wa jamii yetu lakini preassure ya magharibi ilituzidi.

Hakuna aliyejali au kuthubutu kuturudisha kwenye misingi ya malengo yetu ya kudai uhuru na kuuishi uhuru huo.

Leo hii tumempata Rais Mzalendo na aliyelelewa vyema kusimamia tunu za Taifa ...Rais Magufuli.

Rais Magufuli anaturudisha nyuma lakini katika kasi na muktadha wa kisasa kabisa.

Rais Magufuli analiendesha Taifa katika kipindi ambacho kuna wasomi wengi na ambao baadhi wamemezeshwa sumu ya kimagharibi.

Najaribu kuwaza Taifa hili lingekuwa wapi kama tusingempata Rais kama Magufuli.

Hii ni era ya Magufuli kwa manufaa ya wanyonge wengi nchini Tanzania.

Wanaopinga wapo na watakuwepo na wanatakiwa kupuuzwa.
Mission accomplished Mwenyezi Mungu Ailaze Mahala Pema Peponi kazi kwa CCM kufuata nyayo za Marehemu ambaye alijitoa muhanga kurudisha heshima ya CCM na Tanzania kwa ujumla
 
Ningekubaliana nawe asilimia 100 kama KATIBA YA WANANCHI ingepatikana akiwa madarakani. Huo ndio ukombozi kamili
 
Back
Top Bottom