Tusimtukane mtu: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusimtukane mtu:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LD, Nov 23, 2010.

 1. LD

  LD JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jamani tunatakiwa tutambue hivi, CCM ni wajanja, na wanajua kabisa kuna watu ambao wakikamata
  akili zao na maisha yao, itawapa kufanikiwa ktk kuendelea kumtawala Tanzania.

  Tutazame mambo haya;
  * Mkakati wa kuviteka vyombo vya habari eg Clouds...........
  * Kuwateka wasanii eg Malow, Nakaaya ............
  * Kuwateka viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali eg Mama Rwakatare, Mzee Kulola, kuna na huyu wa Siloamu ministry Mnuo anajiita Elia, Mungu nisamehe lakini mafundisho yake mwenzenu siyaelewi, na siku ya uchaguzi aliwaambia waumini wake Kikwete ndo......

  Hebu tujaribu kufikiria, hapo waumini wote wa hawa watumishi wakiambiwa Mungu kasema, wataacha kuchagua CCM.
  Hasa ukizingatia watu wengi wanaokwenda kwene haya makanisa ni wachache sana wenye elimu ya Uraia? (Mnisamehe jamani).

  Huku watu wanafikiria kubarikiwa na Mungu, kwenda Mbinguni, kumkemea shetani na kupigana katika ulimwengu wa Roho.
  Sisemi wanakosea au tunakosea, ila kuna elimu fulani watu wanatakiwa wapatiwe ili waweze kufikiria wenyewe.

  Watu wapewe;
  Elimu ya uraia, wafundishwe wajue haki inapiganiwa sio kwa kuomba tu na vitendo pia, tena tukiongozwa na Mungu, mbona alimwongoza Daudi, Samson, Gidion na wengine?

  Kwa hiyo basi hakuna haja ya kuwatukana sana hawa watu, ila tujue kuna kitu kimefichwa nyuma yao.
  Na Mungu atupe Hekima na Neema jinsi ya kupambana na hizi hila za CCM.

  Kila kinachofanywa na CCM kina maana wakuu, kwa hiyo ni vizuri kuzijua hizi mbinu ili tujipange vizuri.
  Na hali ya maisha tulioyonayo ni nani asiependa kuinuka kiuchumi, kuheshimiwa, na kadhalika?

  Ni vizuri pia kuwaombea hawa watumishi, wakati mwingine hata na wao wanapungukiwa, Ingawa moyo wa mwanadamu aujuae ni Mungu peke yake.

  Tuko vitani jamani, tusiwe wepesi kutukana tu, ila kila kinachotokea tujaribu kuangalia kuna nini nyuma ya jambo hilo?
  Halafu tulifanyie kazi, au tutafute mbinu za kupambana nalo.
   
 2. B

  BA-MUSHKA Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndivyo uonavyo. OK
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Mpwa kusema kweli nimeipenda sana, binafsi sikuelewa na sikupenda alichokifanya mama lwakatare kutumia kanisa kujipongeza kisiasa! kwa nini tulimshambulia Kakobe na kumshangilia Lwakatare? kweli nimeumia sana tena sana, ningekua na uwezo ningelifunga kanisa lile!!!
   
Loading...