Tusimame na Iran na Qatar

Tusimame na Iran na Qatar

Marekani ilishanunuliwa na saud,
hukusikia ule mkwara wa saud kununua silaha marekani za Usd bilion 200?,
hakuna nchi itaachia deal kubwa kiasi hicho,na kazi aliyopewa marekani ni kufanya regime change iran,ili waarabu wajisikie amani,kwani wanahofu persian empire itawameza kama zamani,ukichukulia iran sasa inacontrol iraq,syria,lebanon na kiasi yemen.

Pia waarabu wana hofu na ottoman empire,wanaona Endorgan nae ameanza kueneza himaya yake,
so israel nao wamepewa kazi ya kummaliza endorgan,ndo maana juzi wamemkosa kosa kule bosnia hezgovena
 
Tunasimama na Iran na Qatar, Uonevu Dhidi Yao Si Sawa - Tanzania Tusaidie Amani ya Ulimwengu.

[Sehemu ya Nne na ya Mwisho ya Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB) Juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/19]

Mheshimiwa Spika

Jambo la mwisho kwenye mchango wangu ni juu ya hali ya ulinzi na usalama duniani. Usiku wa kuamkia Disemba 9, 2017, tulipoteza askari wetu 14 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa huko DRC Congo, wakiwa kwenye Jeshi la kulinda Amani la Umoja wa Mataifa. Nachukua nafasi hii kuwaombea kwa Mola awalaze pema, pamoja na kutoa pole kwa familia zao na kwa Jeshi zima la JWTZ. Hawa ni wazalendo waliokufa wakibeba bendera yetu ya amani ulimwenguni.

Taifa letu linachangia pakubwa katika kulinda amani ya ulimwengu, wanajeshi wetu wakiwa karibu katika nchi nane duniani. Naamini tunao wajibu kama Taifa kusaidia uwepo wa amani Ulimwenguni ili kuzuia nchi zilizo kwenye machafuko kama DRC Congo kuongezeka na askari wetu wa kulinda amani kupotea.

Tayari, katika siku za karibuni, dunia imeshughudia maafa makubwa ya vita nchini Libya (ambako Rais Kikwete ni msuluhishi), Iraq, Afghanistan, Somalia, Syria, Sudan Kusini na Yemen. Mwenendo wa migogoro na uonevu unofanyika Qatar na unaotaka kufanyika Iran unapaswa kukemewa mapema ili kuchochea amani ulimwenguni, hasa eneo la mashariki ya kati ambalo tayari limeharibiwa na vita.

Hotuba ya Waziri ya Bajeti ya Wizara hii kwa mwaka 2016/17 ilibeba pongezi kwa nchi za Iran, Marekani, China, Urusi, UN na Umoja wa Ulaya (hasa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani) kwa makubaliano ya Nyuklia yaliyoiondolea vikwazo Iran kwa masharti ya kutoendeleza urutubishaji wa nyuklia. Makubaliano yale ni muhimu kwa kuwa yaliondoa hali ya mashaka iliyokuwa imetanda duniani.

Tumeona Marekani imejitoa kwenye makubaliano hayo, na kutishia kuweka vikwazo vipya kwa Iran. Huku wajumbe wengine wa makubaliano hayo wakiendelea kubaki, kwa kuwa bado Iran imeendelea kutekeleza makubaliano hayo, na kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA ni kuwa bado Iran inafuata masharti ya makubaliano husika.

Uamuzi huu wa Marekani si mzuri, unarudisha hali ya mashaka kwenye eneo la mashariki ya kati, ni uonevu dhidi ya Iran, hasa kwa kuwa IAEA imethibitisha kuwa Iran haina makosa. Ni uamuzi wa uonevu tu na usiochochea amani, ni uamuzi unaopaswa kupingwa. Serikali yetu iitumie nafasi yake kule UN kupinga uamuzi huu, na kuitaka Marekani kurudi kwenye makubaliano haya ili kudumisha amani.

Pia, Julai 26, 2017 Wizara hii ilitoa taarifa yake juu ya mgogoro wa nchi za Ghuba (GCC), baada ya hatua ya nchi nne za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri za kuiwekea vikwazo vya anga, bahari na ardhini nchi jirani ya Qatar. Msimamo wa Serikali yetu ni kuunga mkono upatanishi unaongozwa na Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Jaber, sisi ACT Wazalendo tunaunga mkono msimamo huo.

Lakini bado pia sisi ACT Wazalendo tunasimamia tamko letu la kupinga uonevu dhidi ya Qatar tulilolitoa July 24, 2017. Kwa karibu miezi 10 sasa watu wa Qatar wamewekewa vikwazo vya kiuchumi na kiusafiri, kwenye anga, ardhi na bahari na nchi hizo nne jirani, jambo hilo si sawa, hasa kwa kuwa masharti yaliyotolewa ili kuondoa vikwazo hivyo yanaingilia uhuru wa nchi hiyo.

Tunaitaka Serikali yetu, pamoja na kusapoti usuluhishi huu wa Kuwait, itumie nafasi yake pia kule UN kuhakikisha inachangia usuluhishi wa jambo hili ili mashaka yaliyoko na vikwazo kwa Qatar viondoshwe, ni wajibu wetu huo kama taifa kusaidia amani ya dunia na hivyo askari wetu kutokupoteza maisha wakiwa wanalinda amani kwenye maeneo mbalimbali yaliyo na vita na migogoro.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza. Naomba Kuwasilisha

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bungeni Dodoma
Mei 23, 2018
Zitto mimi ni pro democracy na sifikiri Iran wana nia nzuri. Ukiangalia vizuri middle East kuna matatizo makubwa . Wote Saudi na Iran ni tatizo kwasababu wana nia mbaya ya kuwa na utawala usio wa kidemokrasia. Iran utawala wa Shia na Saudi suni. Atomic bomb ya Iran ni kwasababu tu ya kuzuia mabadiliko ukifikiria vizuri nuklia ya nini wakati wana gas, mafuta etc. Hivyo kama tunataka mabadiliko middle East ni kukataa muundo wa utawala wa Saudi na Iran kwa ujumla na sio kuwa upande mmoja maana wote ni tatizo. Nchi ambayo wanawake wanafanya kama bidhaa tu sio utamaduni tunaoutaka kwa dunia ya leo kwa kweli.
 
Vilevile kwenye nchi nyingine kama Libya mabadiliko yanachukua muda, watu kubadilika kunachukua muda, hata demokrasia zetu mwanzo zilionekana bora wazungu sio
 
Ya kwetu yametushinda ya wenzetu yanatuhusu nini? wapamabane na hali zao nasi tupambane na yetu:
demokrasia ya kweli hakuna
uonevu
kubambikia wapinzani kesi za uongo
Wizi wa kura
gilba
fitna
upendeleo
ukanda nk
 
Marekani ilishanunuliwa na saud,
hukusikia ule mkwara wa saud kununua silaha marekani za Usd bilion 200?,
hakuna nchi itaachia deal kubwa kiasi hicho,na kazi aliyopewa marekani ni kufanya regime change iran,ili waarabu wajisikie amani,kwani wanahofu persian empire itawameza kama zamani,ukichukulia iran sasa inacontrol iraq,syria,lebanon na kiasi yemen.

Pia waarabu wana hofu na ottoman empire,wanaona Endorgan nae ameanza kueneza himaya yake,
so israel nao wamepewa kazi ya kummaliza endorgan,ndo maana juzi wamemkosa kosa kule bosnia hezgovena
There are still many we will see

let's just wait time will tell
 
Wakristo wengi wanatetea wayahudi japo si dini yao lakini kutokana na umbumbumbu uliojaa miongoni mwetu tunashindwa kutofautisha. Wale ni wayahudi wakatili wanatesa wapalestina na watu wanafumba macho. Laaanatullah alayhim
 
Sijasoma maelezo yote ya post ya kwanza ya uzi huu, lakini ningependa kuwafahamisha wanaJF kuwa ninashauri kwa ,wakati huu, Serikali yetu ijikite kwenye kutekeleza yale tu ambayo yamekubaliwa na mamlaka halali za kimataifa yaani yaliyomo kwenye UN charter na yale yaliyokubaliwa na UNSC kama 'resolutions'. Suala la mashariki ya kati kwa wakati huu pia ni 'volcano inayofukuta' na ikilipuka inaweza kuizamisha sehemu kubwa ya dunia hii. Hivyo hatutakiwi kuchezea karibu na fukuto hili la volcano. Kwa maneno mengine...ule utaratibu wetu wa kutokuwa na upande ni muhimu sana. Non-aligned movement ni muhimu wakati huu wakati tukitekeleza yale yaliyokubaliwa na mamlaka halali za kimataifa.
 
Iran na Qatar wanatusaidia nini...tunasimama nao wa nini hasa! Zitto kapambane mkoa wa kigoma watu wasome, wale vizuri, wawe na nyumba nzuri, wavae vizuri na watibiwe vizuri basi. Mengine kaa kimya
 
Wakristo wengi wanatetea wayahudi japo si dini yao lakini kutokana na umbumbumbu uliojaa miongoni mwetu tunashindwa kutofautisha. Wale ni wayahudi wakatili wanatesa wapalestina na watu wanafumba macho. Laaanatullah alayhim
We unaeleta dini humu ndio huna akili kabisa. Hio research umefanyia wapi unaleta mihemko hapa! Dini yako hainisaidii wala yangu hakusaidii. Imani za wakoloni ambazo umekopi na kubandika kichwani mwako zimekufanya akili igande.
 
Acha kujichanganya ndugu yangu!
 
Iran na Qatar wanatusaidia nini...tunasimama nao wa nini hasa! Zitto kapambane mkoa wa kigoma watu wasome, wale vizuri, wawe na nyumba nzuri, wavae vizuri na watibiwe vizuri basi. Mengine kaa kimya
True
 
We unaeleta dini humu ndio huna akili kabisa. Hio research umefanyia wapi unaleta mihemko hapa! Dini yako hainisaidii wala yangu hakusaidii. Imani za wakoloni ambazo umekopi na kubandika kichwani mwako zimekufanya akili igande.
Hahahaha
 
Zitto atetee democracy ktk nchi kwani hata yeye hapo alipo, kwa jukumu lake kama mpinzani, hajui kwa uhakika kama ataiona siku ya kesho..

Hawa sijui Iran, Qatar nk hawana kabisa muda na mambo yetu wala hata Ebola ikituvamia leo, hatutawasikia kamwe labda wasikie waislamu kadhaa wameshambuliwa msikitini, ndio watashindana kulaani.

Nchi kama South Africa, Mozambique nk leo wanajiona wako huru kwa ajili ya sisi kuwafia lkn leo Mtanzania akiwa kwenye nchi hizo ni mgeni au adui kuliko Mkenya aliyeko huko....!!!! In short, ya nje hayatuhusu saaana kihivyo kama na yetu yasivyowanyima usingizi.
 
Back
Top Bottom