SoC04 Tusilazimishe matumizi ya TEHAMA pekee kama miundombinu bado, TEHAMA bila miundombinu toshelevu ni kero kubwa kwa wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Xpertz

Member
May 3, 2024
11
8
UTANGULIZI
Miaka ya karibuni kumekua na kampeni na kiu kubwa ya wananchi, Serikali na Sekta binafsi kutumia TEHAMA kama njia kuu ya kuwezesha huduma kirahisi na kwa haraka, ila changamoto kubwa ni kwamba bado miundombinu wezeshi ya TEHAMA nchini Tanzania hususan maeneo mengi ya vijijini sio rafiki. Mtandao haukamati na kwa bahati mbaya taasisi nyingi zimeanza kulazimisha wananchi kupata huduma kupitia TEHAMA pekee kwenye mitandao yao ya wavuti(website) nk.

Mfano ni tangazo la ajira za jeshi la polisi nchini Tanzania zilizotangazwa tarehe 9 Mwezi wa 5 mwaka 2024 ambapo jeshi hilo lilielekeza waombaji wote kutuma maombi yao kwenye wavuti yao (Police Recruitment Portal) ambayo kwa wakati wote wa maombi mfumo wao wa kupokea maombi (server) ulikuwa haufanyi kazi na kuwa kero kubwa kwa wananchi mpaka bunge kutaka Serikali itoe tamko.

Mfano mwingine ni mfumo wa Ofisi ya Rais utumishi kwenye suala la taarifa za Mpango kazi wa Watumishi na utekelezaji wa majukumu yao maarufu kama PEPMIS, mfumo huo ni mzuri ila changamoto ni kubwa mno kwa Watumishi walio maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa mtandao ni changamoto kubwa hata simu janja hazishiki mtandao Watumishi wa maeneo hayo wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kujaza taarifa hizo maeneo yenye mtandao hususan mijini hivyo kuingia gharama kubwa ya nauli na hata kulipia kwenye vibanda vya TEHAMA. Nini kifanyike kuboresha huduma za TEHAMA bila kuwa kero kwa wananchi?

1. Nashauri taasisi za Serikali na binafsi zisilazimishe wananchi kupata huduma kupitia TEHAMA pekee, kuwe na chaguo la nakala ngumu na laini(softcopy) ili kuwapa unafuu watu walio mazingira yenye changamoto kubwa ya mtandao hususan vijijini mpaka huduma ya upatikanaji wa mtandao itakapokua imeimarika kwa usawa maeneo yote ya nchi. Kwa kifupi matumizi ya TEHAMA maeneo mengi ya vijijini mfano kijiji cha Nimbo wilayani Kahama halmashauri ya Ushetu, Uvinza na Kibondo mkoani Kigoma, Tingi-Nyasa na maeneo mengi ya Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Madaba huduma ya mtandao iko chini mno.

2. Serikali ITUMIE miundombinu ya kisasa ya TEHAMA hususan satellite, hapa nashauri wawekezaji wa huduma za mtandao wa kimataifa wenye UFANISI mkubwa na teknolojia ya kisasa zaidi kama kampuni ya Star Link wapewe nafasi ili kurahisisha matumizi ya TEHAMA nchini kwa UFANISI na unafuu. Serikali kwa sasa inasema inategemea viwezeshi vya kebo za baharini miundombinu ambayo imepitwa na wakati na haina kasi wala ubora kama ilivyo kwa satelaiti(satellite). Tumeona changamoto ya miundombinu hiyo ya kizamani ilivyosababisha kero kubwa ya kukosekana mtandao nchini mwanzoni mpaka katikati mwa Mwezi wa 5 mwaka 2024.

3. Huduma za TEHAMA ziboreshwe hususan maeneo ya vijijini ambako bado changamoto ni kubwa mno. Kwa mfano huduma ya ATM mkoa wa Shinyanga ni kama mabenki yameamua kuhujumu wateja kwa makusudi kabisa kwakua wanajua iwapo ATM zikiwa chache wananchi watalazimika kutumia mawakala wao kutoa fedha njia ambayo ni gharama zaidi kwa mteja.

Mfano halmashauri ya Manispaa ya shinyanga kuna ATM za CRDB Benki tatu pekee na mara nyingi ile iliyopo eneo la stendi ya zamani inakua mbovu au haina fedha na kusababisha kero kubwa kwa wananchi kwenda kukaa foleni kubwa mno kwenye ATM za pale pale Benki mtaa wa NSSF ya zamani. Huku ni kukwamisha kwa makusudi juhudi za Serikali kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa wananchi dhamira njema iliyokua na lengo la kuwarahishishia huduma sambamba na kuwapa unafuu.

4. Elimu ya msingi ya TEHAMA itolewe kwa jamii sambamba na kuboreshwa udhibiti kuzuia uhalifu wa ki TEHAMA. Matumizi ya TEHAMA nchini kwa kiasi kikubwa yamekuja na kupokelewa moja kwa moja na jamii bila elimu ya kutosha kuhusu matumizi sahihi ya TEHAMA. Mfano mzuri ni wimbi kubwa la matapeli wa kimtandao wanaojitwalia ushindi kwa kufanikiwa kutapeli watu wengi kupitia TEHAMA na kusababisha hasara na vilio kwa maelfu ya wananchi kila siku ikiwemo wastaafu. Ni dhahiri matapeli na wahalifu hao wa kimtandao wanatumia mwanya wa uelewa mdogo wa jamii kuhusu TEHAMA na matumizi yake kwa ujumla.

Mamlaka ya teknolojia na Mawasiliano TCRA iongeze nguvu kubwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya TEHAMA sambamba na tahahdhari kuhusu mbinu wanazotumia wahalifu kufanya uhalifu wa kimtandao. Nitoe pongezi kwa baadhi ya taasisi za umma pia ambazo zipo mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu namna matapeli wa kimtandao wanavyotumia TEHAMA kuwatapeli wateja wao mfano mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF na jeshi la polisi Tanzania. Nashauri elimu hiyo itolewe na taasisi na mashirika yote kwa nguvu. Pia vyombo vya habari vitumike kutoa matangazo ya tahadhari kuhusu matapeli wa kimtandao sambamba na kuendesha mijadala mingi ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya TEHAMA.

Nawasilisha.
 
2. Serikali ITUMIE miundombinu ya kisasa ya TEHAMA hususan satellite, hapa nashauri wawekezaji wa huduma za mtandao wa kimataifa wenye UFANISI mkubwa na teknolojia ya kisasa zaidi kama kampuni ya Star Link wapewe nafasi ili kurahisisha matumizi ya TEHAMA nchini kwa UFANISI na unafuu. Serikali kwa sasa inasema inategemea viwezeshi vya kebo za baharini miundombinu ambayo imepitwa na wakati na haina kasi wala ubora kama ilivyo kwa satelaiti(satellite). Tumeona changamoto ya miundombinu hiyo ya kizamani ilivyosababisha kero kubwa ya kukosekana mtandao nchini mwanzoni mpaka katikati mwa Mwezi wa 5 mwaka 2024.
Kweli, tuwe na miundombinu ya kisasa inayowezesha kuibeba hiyo mifumo yote ya tehama.

Ile habari ya 'Mtandao unazingua, ifutike kabisa'🙅‍♂️

Nawasilisha
Nzurri👏
 
Back
Top Bottom