Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,273
- 21,455
Nashangaa kwamba wengi wa Watanzania ni wenye kulalamika kila kukicha juu ya uongozi wa Magufuli bila kusema tatizo ni nini. Wengi wanasema tu amefanya hali iwe ngumu nchini, kauli ya kiujumla sana. Wapo wachache wenye kusifia. Sasa kulalamika au kusifia bila kutaja mambo halisi haitusaidd chochote. Kama kweli tuna kitu cha kumlalamikia Magufuli, au kumsifia, basi acha tuorodheshe kwenye uzi huu yale tunayoona ni mabaya au mazuri aliyofanya ili ieleweke wazi kwake Magufuli au kwa wengine.
Endeleza uzi huu kwa kuorodhesha mazuri au mabaya unayoona juu ya Raisi Magufuli. Hiyo itasaidia sana badala ya kulalamika au kusifia bila kuwa wazi.
Mie ninaanza.
Mazuri:
1. Ujenzi wa barabara za kutumika kwa faida ya wengi na kwa muda mrefu kwa kutumia fedha za sherehe ambazo zingetumika kwa siku moja kwa faida ya wachache
2. Kujenga nidhamu ya kazi na uwajibikaji kwa muda mfupi aliokuwa madarakani
3. Wanafunzi kusoma bure
4. Kuongeza kwa kiasi kikubwa utengenezaji wa madawati ya watoto wetu shuleni
5. Kudhibiti kukwepa kodi bandarini
6. Kuondoa viongozi wazembe wasiochapa kazi na wenye harufu ya ufisadi bila kuwaonea aibu
7. Kupunguza gharama za idara za serikali zisizo za msingi
8. Kuja na mpango kabambe wa daraja toka Kigamboni hadi Kunduchi kwa gharama chini ya lile la Kigamboni
9. Kuhuisha shirika la ndege la Tanzania
Mabaya
1. Kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani na kwa ujumla kuwa na ushirikiano mdogo sana na vyama vya upinzani na hata kutotambua mchango wao kwa Tanzania
2. Kutumbua baadhi ya viongozi bila kufanya utafiti wa kina (mfano, Meneja wa Tanesco)
3. Kutumia nguvu za kijeshi (hasa polisi) kwa kiwango kinachozidi mpaka na kwa makosa madogo madogo yenye mtazamo wa kisiasa
4. Kufumbia macho baadhi ya ufisadi mkubwa nchini (Alama za vidole, Meremeta nk) bila kutueleza sababu kwa nini hatua hazijachukuliwa
5. Kufanya uteuzi mwingi kwa ngazi za mikoa na wilaya kwa mtazamo wa kisiasa badala ya kuitalaamu
6. Kuwapa wakuu wa wilaya na mikoa mamlaka makubwa yasiyo ya kikatiba na kuleta mgongano wa kiutendaji na serikali za mitaa (mfano, Mkurugenzi/Madiwani Vs Mkuu wa Wilaya), na hata wananchi na hivyo kukwamisha mipango ya maendeleo katika mikoa na wilaya
7. Kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari
8. Kutokuwa mwangalifu katika kutoa matamko, maagizo au amri ambazo zina mtazamo wa kuvunja katiba ya Tanzania aliyoapa kuilinda