Tusikimbie tatizo katika Elimu

Prispian

Member
Jan 22, 2017
33
39
Wiki hii matokeo ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka jana yametangazwa. Kuna shule zinasherehekea na nyingine zina simanzi. Shule takribani sita za mkoa wa Dar ni miongoni mwa shule zilizoshika mkia. Wizara ya elimu iko hapo, wakaguzi wa mashule wako hapo, vitabu vinachapishwa hapo, kila aina ya miundombinu iko hapo. Sio mbaya kuwa wa mwisho lakini kwanini mashule ya serikali na hususani shule za kutwa? Jambo la ajabu sana anakwenda kuulizwa na kushushwa vyeo mwalimu ama anatimuliwa ama anahamishwa. Kwa shule za kutwa mtoto anasoma nyumbani sio shuleni, pale shuleni anafundishwa tu. Muda wa kujisomea anaupata nyumbani sio shuleni. Kwa mantiki hiyo wazazi wanawanyima ushirikiano watoto wao huko nyumbani kwa kuwajazia kazi nyingi za nyumbani badala ya kuwapa muda wa kusoma. Tusipowaelewesha wazazi kuhusu hili, tutafukuza walimu wote na hali itaendelea kuwa vilevile. Naomba wazazi washirikiane sana na walimu kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi mara kwa mara. Walimu ni walewale, vyuo walivyosoma ni vilevile, watoto ni hawahawa wa kitanzania, kwanini Private na boarding government wanafaulu vizuri? Wazazi tushirikiane na walimu wetu ili kuwanusuru wanetu.
 
Mada kama hii eti haina wachangiaji mpaka muda huu, Siasa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom